2.0
Taarifa hii si ya ukweli na ni ya upotoshaji,Mhe Jaji Mkuu hajawahi kuzungumzia
chochote kuhusu sheria hiyo ukitilia maanani kesi hiyo iko Mahakama Kuu shauri
Namba 37 ya 2015 iliyofunguliwa na Bi. Amy Kibatala dhidi ya Mwanasheria Mkuu
wa Serikali (AG) na Mkurugenzi wa Uchaguzi (DE) na itatolewa maamuzi kati ya
tarehe 22 au 23 mwezi huu. Hivyo, kwa mujibu wa sheria Mhe.Jaji Mkuu asingeweza
kuzungumzia chochote kuhusu sheria hiyo kwa kuwa suala hilo liko MAHAKAMANI.
3.0 Tulimwandikia Mkurugenzi wa Habari MAELEZO nakala East Africa Television
na kufuatilia kwenye Baraza la Habari (Media Council) kuomba maelezo ya kina na
usahihi wa taarifa hiyo, tarehe 21/10/2015 tumepokea barua Kumb Na EATV/ADMN/096/10/2015 ilyosaniwa na Bi Regina
Mengi Mkurugenzi Mtendaji wa East Africa Television akiomba msamaha kuhusu
taarifa hiyo potofu na kuwa watatoa maelezo ya ziada kuwa, taarifa hiyo
haikutolewa na Mhe.Jaji Mkuu wa Tanzania
Tunashukuru kwa ushirikiano mkubwa
tulioupata toka uongozi wa juu kabisa wa East Africa Television kwa kuomba
radhi mapema na Tunamini kuwa, vyombo vya Habari na Wananchi kwa ujumla vitasitisha
usambazaji wa taarifa hii iliyokuwa si sahihi.
Barua ya kuomba radhi
imeambatanishwa:
Imetolewa na:
MTENDAJI MKUU WA MAHAKAMA
MAHAKAMA YA TANZANIA
Tumesha zoea kulishwa uongo hata hilo hatuwezi kuliamini.kuna redio moja asubuhi kuna mtangazaji anajifanya shabiki wa chama fulani anasema mahakama tu ndoinaweza kutafsili.kusoma hajui nata kusikiliza hawezi.yaani uchaguzi huu umenipa elimu sana.nimejua mtanzania ni nani na yukoje.inasikitisha sana.
ReplyDeleteMungu atusaidie.elimu tulizopata zitusaidie.
Hii ni hatari kubwa hii TV siamini tena maishani mwangu na ni bora ifungiwe maisha ndugu zangu watanzania jirani zetu walianza na mambo kama haya matokeo yake MOTO uliowaka walishindwa kuuzima na kusababisha mauwaji ya kinyama mcheka na nyani huvuna mabuwa
ReplyDelete