Huu ni uchambuzi wa Habari toka vituo mbalimbali vya Televisheni Usiku Huu October 18, 2015.
Spika wa Bunge la Tanzania Anne makinda na Viongozi wa Vyama na serikali washiriki katika mazishi ya Mbunge wa Ludewa Marehemu Deo Filikunjombe. https://youtu.be/p_E20X5YaNE
Wastani wa wanawake milioni 1 duniani huugua wa saratani huku asilimia kubwa ya vifo vya wanawake hutokana na saratani ya shingo ya kizazi. https://youtu.be/ytCtaSi6qJs
Waziri mkuu Mizengo Pinda amewaasa viongozi wa serikali kushiriki katika Ibada na kujitokeza kusaidia makundi mablimbali yenye mahitaji maalumu. https://youtu.be/yOMPgmrgBbs
Mgombea Uraisi CCM Dkt John Magufuli aahidi kuboresha kilimo cha pamba nchini iwapo atachaguliwa kuongoza serikali ijayo ya awamu ya 5. https://youtu.be/MBuzgeCq3UY
Alpha Conde ashinda uraisi Guines kwa asilimia 58 ya kura dhidi ya mpinzani wake Dialo aliyeapa kujitotokeza kupinga matokeo hayo. https://youtu.be/pEHDriV1slw
Mgombea Mwenza CCM Bi. Samia Suluhu awaahidi wananchi Mbeya kuboresha miundombinu ya barabara ili kurahisisha usafirishaji wa bidhaa za Biashara. https://youtu.be/I8WK1WGyX-k
Viongozi Wa Dini kote nchini wametakiwa kuendelea kuliombea taifa katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu oktoba 25. https://youtu.be/azFOsCgMoVM
Baadhi ya makocha nchini wamejitokeza na kuwapa mazoezi ya Pamoja wasichana wadogo na wavulana katika harakati za kukuza soka la wanawake. https://youtu.be/FA2AMfCFS_o
Kalbu Ya Soka Coastal Union imekiri kukabiliwa na wakati mgumu kutokana na kuvurunda na kupokea vipigo mechi za ligi kuu. https://youtu.be/Yhx-bmpB6MM
Baraza la waislamu BASATA Mwanza lalaani vikali taarifa zilizozagaa mitandaoni juu ya Askofu Gwajima kuua Dini ya kiislamu Tanzania. https://youtu.be/v6ZFqn1iJec
Wakulima wa Zao la nafaka Hai mkoani Kilimanjaro wameiomba serikali kuhakikisha inatoa mikopo ya pembejeo za kilimo ili kuongeza uzalishaji. https://youtu.be/OBAuNAGU8kI
Kamati inayoongoza soka visiwani Zanzibar hapo kesho itakutana na wakuu wa shirikisho la soka TFF kuelezea juu ya maendeleo ya soka Zanzibar https://youtu.be/PEJBPEnxtcw
Makamo Wa Raisi wa Tanzania Dkt. Gharib Bilal awataka wananchi kuzingatia usafi wa mazingira na kutunza miradi ya maendeleo. https://youtu.be/5oZMazN_Q1Q
Wanafunzi wenye ulemavu katika shule ya Msingi Kizenga mkoani singida wahitaji msaada wa vifaa vya kufundishia na kukosa Chakula. https://youtu.be/6ntRfFsF6Ns
Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA limefanya droo ya upangaji ratiba kwa mechi za awali za mtoano kufuzu mashindano ya Ubingwa barani ulaya. https://youtu.be/BzMWK0Em8qQ
Mama Anna Mgwira ajibu sababu ya kwa nini anaona anafaa kuwania nafasi ya kuwa Raisi mwanamke wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania. https://youtu.be/mVWYXU_3xFo
Hiki ndicho kinachoendelea katika mdahalo maalumu wa wagombea uraisi wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndani ya Kipindi Cha MKIKIMKIKI. https://youtu.be/kvnyF_wIFhE
Wafahamu Wagombea Walioalikwa ndani ya mdahalo maalumu wa wagombea uraisi sanjari na vigezo husika ndani ya Mdahalo huu. https://youtu.be/BBIzZGYFuXs
Haya ndiyo Majibu Ya Mgombea Uraisi ADC juu ya swali la kwa nini anaona anafaa kugombea nafasi ya Uraisi wa Tanzania. https://youtu.be/CG6O-R1eICA
Je ni kwa namna gani wagombea uraisi hawa endapo wakifanikisha kuingia madarakani watakomesha suala zima la Ufisadi na Rushwa? https://youtu.be/peqhV4ee6k8
Ni nini suluhisho la rushwa kwa vijana wahitimu wa vyuo mbalimbali wanaokosa nafasi za kazi kwa kigezo cha uzoefu kazini? Chief Yemba anajibu. https://youtu.be/5ZhsE0Ib1-E
Dkt Magufuli awataka wananchi wa Misungwi kuibeba kiuchumi na kimaendeleo endapo atapata ridhaa ya kuwa raisi wa Tanzania. https://youtu.be/Q3ypq5Cua7w
Utekelezaji wa ahadi za wagombea wanazoahidi wagombea majukwaani zinatolewa ufafanuzi na wagombea waliohudhuria mdahalo maalumu leo. https://youtu.be/j6gWs_VUHk4
Dkt. Magufuli awaomba wananchi wa Misungwi kutumia ipasavya Miundombinu ya barabara katika masuala ya Biashara na kuinua Uchumi. https://youtu.be/1b8xtO9WikU
Mgombea Uraisi CCM Dkt. Magufuli awahakikishia wananchi kuhusu suala la maji na Umeme na kutoa mikopo kwa akina mama kujikwamua kiuchumi. https://youtu.be/mO5_GFMHZm4
Dkt. Magufuli atoa ufafanuzi juu ya uboreshaji wa mishahara ya walimu, wafugaji na wakulima kuondolewa ushuru usio wa lazima. https://youtu.be/GfuznXDD4E8
Dkt Magufuli amnadi Mgombea Ubunge Misungwi Ndg Kitwanga kwa maendeleo yakinifu wa wananchi wa Misungwi na Taifa zima la Tanzania. https://youtu.be/H94X9XJTkKM
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...