Msikiti mpya wa Kitongoji cha Kimbangulile, Mkuranga Pwani
Msikiti wa zamani wa Kitongoji cha Kimbangulile Wilaya ya Mkuranga mkoni Pwani.
Zaidi pia Mungu awabariki waendeshaji wa blog hii ya Jamii kwa kutuunga mkono katika kupeleka habari kwa Jamii na kutuunga mkono katika harakati zetu.
Ndugu zangu Wapendwa Michango tuliyo kusanya toka mwanzo Program PROJECT zetu za kheri hizi ni Tshs 6,000,000 ( Milioni Sita ) .
Pesa hizi zimetumika katika kuwezesha kufanya Mambo Mawili katika sehemu tofauti , Sehemu ya Kwanza ni Mkoa wa Pwani , Wilaya ya mkuranga , Kijiji cha Mlamleni , kitongoji cha Kimbangulile hapa tumewezesha kuubadilisha ki ujenzi Msikiti kutoka katika hali ya Nyasi kuwa hali ya bati kama mnavyo ona katika Picha .
Masha Allah! si haba Alhamdulillah. Jazakallahu Khayra kwa kila aliyetoa chochote kile ima kwa hali ama mali katika kulifanikisha jambo hili la kheri, kwani kufanya mambo kama haya ndizo 'Swadaqatin'jariya' zenyewe zinazotakiwa. Mwenyeez Mungu azidi kutujaaliya kwa yeyote mwenye moyo wa kutowa ama kusaidia kwa njia moja au nyingine katika kulikamilisha jambo hili la kheri (ujenzi huu wa Mskiti) basi tusisite, kwani jaza yetu tutakwenda kuikuta kesho huko usoni twendako, In Sha Allah.
ReplyDelete