![]() |
Katibu Mkuu wizara ya Maji,Mhandisi Mbogo Mfutakamba akizungumza wakati wa kuzindua Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Saalam(Dawasa) jijini Arusha. |
WAZIRI wa Maji,Profesa Jumanne Maghembe amezindua Bodi mpya ya
Wakurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam(Dawasa) na kuitaka kuhakikisha wanafanyakazi kwa bidii katika mfumo wa Matokeo Makubwa Sasa ili kuondoa kero ya maji kwa wananchi.
Maghembe alitoa kauli hiyo jijini Arusha na kusema kuwa serikali imepata kiasi cha dola za Marekani 409 kutoka Benki ya Dunia,Korea Kusini na wadau wengine kuweka miundombinu ya majitaka itakayosaidia kupunguza uchafuzi wa mazingira kwenye bahari ya Hindi.
Alisema idadi ya watu katika jiji la Dar es Salaam inaongezeka kila mara hiyo serikali imejipanga kuhakikisha inatengeneza miundombinu itakayowezesha upatikanaji wa maji safi na maji taka unaondana na hadhi ya jiji.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...