Meneja uhusiano wa Airtel
Tanzania Jackson Mmbando (katikati) akiongea
na mshindi aliyepatikana wakati wa kuchezesha droo kubwa na ya mwisho ya promosheni ya
"Jiongeze na Mshiko" ambapo bw. Sylvester Lucas Boyo, mwanafunzi na mkazi wa Shinyanga alijishindia shilingi
milioni 50 na Juma Sekele Maruka, Mwalimu mkazi wa Nyakato
Mwanza wateja wawili wa Airtel waliibuka
washindi. (kushoto) ni mkaguzi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha
bwana Humudi Abdul Hussein
na Afisa huduma za ziada Airtel bwana
Fabian Felician.(kulia) droo hii imechezwa jana katika makao makuu ya
Airtel Moroco jijini Dar es saalam.
Afisa huduma za
ziada Airtel bwana Fabian Felician akichezesha droo kubwa na ya mwisho ya promosheni ya
"Jiongeze na Mshiko" ambapo bw. Sylvester Lucas Boyo, mwanafunzi na mkazi wa Shinyanga alijishindia shilingi
milioni 50 na Juma Sekele Maruka, Mwalimu mkazi wa Nyakato
Mwanza wateja wawili wa Airtel waliibuka
washindi. Wakishuhudia ni Meneja
uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando (kulia) na mkaguzi kutoka
bodi ya michezo ya kubahatisha bwana Humudi Abdul Hussein (kushoto).
• Zaidi ya milioni 100 zatolewa ndani ya
siku 120
Dar es Salaam, Jumanne Novemba 10,
2015, Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imewatangaza washindi wa
droo kubwa na ya mwisho ya promosheni ya “Jiongeze na Mshiko”
Airtel imekuwa ikiendesha promosheni ya “Jiongeze
na Mshiko” kwa muda wa siku 120 zilizopita na kuwazawadia wateja wake
wa kila wiki wa milioni 1 kwa ngazi ya Free/BURE na shilingi milioni 3 kwa
wateja wa ngazi ya premium kwa gharama ushiriki wa Tshs300 tu kwa siku.
Leo “Jiongeze na Mshiko” imemzawadia Sylvester Lucas Boyo, mwanafunzi na mkazi wa
Shinyanga , shilling milioni 50 baada ya kuibuka mshindi wa droo kubwa ya
mwisho wa promosheni hii.
Akizungumza wakati wa droo hiyo ya mwisho,
Meneja wa Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando alisema, "leo
tumefikia tamatati ya promosheni yetu ya “Jiongeze na Mshiko” ambapo
mpaka sasa imezawadia wateja wetu zaidi ya shilingi milioni mia moja nchi
nzima. Promosheni hii imeweza kubadilisha maisha ya wateja wetu kwa kuwazawadia
pesa taslim kila wiki.
"Napenda kuwashukuru sana wateja wetu
wote walioweza kushiriki katika promosheni hii ya “Jiongeze na Mshiko” tangu
ilipozinduliwa mwezi Julai mwaka huu. Tunaahidi kwamba Airtel itaendelea
kuwajali, kuwawezesha na kuwazawadia wateja wetu kila siku. Tutaendelea
kuhakikisha tunafungua milango zaidi ya bahati kwa wateja wapya na waliokuwepo,
"alisema Mmbando
Promosheni ya Jiongeze na Mshiko inaonyesha
dhamira ya Airtel katika kujali wateja wake na kuwawezesha watanzania kutimiza
ndoto zao, aliongeza Mmbando.
Airtel pia imemzawadia Juma Sekele Maruka,
Mwalimu mkazi wa Nyakato Mwanza shilingi milioni mbili ambaye aliibuka mshindi
wa mwisho wa ngazi ya Free wa promosheni hii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...