Mkuu wa wilaya ya kinondoni, PAUL MAKONDA anatarajia kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa  chama cha wapishi wa keki nchini kitakachojulikana kama  TANZANIA CAKES BAKERS ASSOCIATION.


Akizungumza na  waandishi wa habari  jijini DSM, mwenyekiti wa muda wa umoja huo PHILIP MBONDE amesema umoja huo utaweza kuwaunganisha wapishi wa keki na wanaojishughulisha na biashara ya cake nchini na kuweza kujumuika pamoja katika majukumu mbali mbali.


“ Hili ni jambo jipya hapa nchini, wapo wajasiriamali wengi katika sekta hii ya keki lakini imekuwa haipewi umuhimu sana ijapokuwa watu wengi wamekuwa wakitumia keki katika shughuli zao mbali mbali,sasa tumeona tuanzishe umoja huu tunajua utaleta tija” alisema Mbonde.


Pia mbali na mkuu w awilaya huyo MAKONDA, mfanyabiashara maarufu wa mau na upambaji nchini CYTHIA HENJEWELE naye atajumuika na wapishi hao ambao wanatarajhia nae aweze kutoa elimu ya ujasiriamali itakayowasaidia wanachama hao.


Mbonde amesema kwamba katika uzinduzi huo wanategemea mkuu wa wilaya MAKONDA kuweza kutoa changamoto kwa wananchama wa umoja huo kutokana na yeye kuwa kijana mwenye  kuthamini sana kazi za wajasiria mali na kujitolea katika kuhakikisha watu wanaweza kufanikisha ndoto zao katika maisha yao ya kila siku.


Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo,amesema umoja huo unatarajiwa kusajili  ili kuwezesha wapishi wote wa keki kuweza kupata fursa za kupata mikopo kutoka katika taasisi za benki ili kuweza kuendeleza biashara zao na kuchangia pato la taifa kwa kulipa kodi na kutoa ajira kwa vijana wa kitanzania ambao hawana ajira.


Mbonde amesema mpaka sasa umoja huo unawanchama hai jumla ya hamisini ambao wanatarajiwa kushiriki katika uzinduzi huo utakaofanyika DSM ambaoi utajumuisha wanachama kutoka mikoa mbali mbali ya TANZANIA.


Amewaomba wadhamini mbali mbali kujitokeza kudhamini uzinduzi huo wa chama chao kipya ambacho wanaimani kitaweza kusaidia wapishi wa keki kuleta tija katika kazi zao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...