Ofisa Mtendaji wa Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam (Dawasco), Mhandisi Cyprian Luhemeja, akizungumza katika mkutano na wafanyakazi uliofanyika hivi karibuni Makao Makuu ya Dawasco jijini Dar es Salaam kuhusu utendaji kazi wa kazi.
Wafanyakazi wa Dawasco wakimsikiliza Ofisa Mtendaji
Mkuu wao.
Na Dotto Mwaibale
Ule usemi maaarufu wa "Hapa kazi tu"unaendelea kuimbwa na
kufanyiwa kazi na Watanzazia wengi hususani watumishi wa Umma na serikali ili
kuendana na kasi ya awamu ya Tano ya Raisi Magufuli. Kauli mbiu hiyo
imekumbushwa tena na Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco Mhandisi Cyprian Luhemeja wakati
wa kikao cha pamoja na wafanyakazi wa
shirika hilo mapema wiki hii.
“Lazima tuendane na kasi na speed ya Mheshimiwa Rais, tabia ya
kufanya kazi kwa mazoea, kutojali malalamiko ya Wateja sasa ni mwisho”
alisisitiza Mhandisi Luhemeja.
Aliwataka wafanyakazi kujali muda wao wa Kazi kwa kutenda yale
ambayo yataondoa kero ya Maji kwa Wateja hususani kuziba mivujo ya Maji katika
maeneo mengi ya Jiji pamoja na kupambana na wizi wa Maji ili kila mwananchi
apate huduma ya Maji kihalali.
Alimalizia kwa kuwataka wafanyakazi wa DAWASCO kutekeleza kauli
ya Rais aliyoitoa mapema wakati akifungua Bunge katika sekta ya Maji pale
aliposema “LAZIMA TUWATUE KINA MAMA NDOO KICHWANI” kwa kuhakikisha huduma ya
Maji inamfikia mwananchi na kuondokana na malalamiko ya upatikanaji huduma hiyo
kwa maeneo stahili.
Wakuu wa Dawasco, nawapongeza kwa kugundua kuwa munapaswa kwenda na kasi iliyoko sasa. Katika kuangalia hilo, naomba muangalie uwezekano wa kusambaza maji eneo la Salasala kwa Abarikiwe. Haituingii akilini sisi wakazi wa huko kukosa maji, ilihali wakazi wa salasala ya mbuyuni wao wanapata majim 24hrs. Tatizo ni nini mpaka kukosekane huduma ya maji kwa eneo hilo. Tunashawishika kuamini kuwa hayo magari yanayouza maji ni ya kwenu au mna share huko.
ReplyDeleteTunaomba mtusaidie tupate hiyo huduma ya maji. Mimi mkaazi wa Salasala - Abarikiwe