KATIKA kutekeleza kauli mbiu ya Rais wa tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,John Magufuli ya “Hapa Kazi tu” serikali mkoani Kilimanjaro imetangaza kusitisha likizo na ruhusa zote kwa watumishi wake katika kipindi cha siku kuu za Krismasi na mwaka mpya.

Agizo hilo linakuja wakati tayari baadhi ya watumishi wa serikali kuanza taratibu za kuomba likizo na ruhusa kwa ajili ya kwenda kushiriki siku kuu za mwisho wa mwaka za Krismasi na mwaka mpya.

.Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Amos Makala alitangaza uamuzi huo jana wakati wa kikao cha kazi alichoitisha na wakuu wa wilaya zote za mkoa, wakurugenzi, kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa na watendaji wengine wa serikali.

“Mh Rais ametoka kwenye kampeni hajapumzika,Makamau wa rais ametoka kwenye kampeni hajapumzika ,Waziri mkuu pia vivyo hivyo sasa sisi ni nani twende kwenye mapumziko ya siku kuu ya Krismasi.”alihoji Makala.

“Kwa maana hiyo ili haya tunayotaka ya elimu bure ,kukabiliana na Kipindupindu ,kwa madaraka niliyopewa kama mkuu wa mkoa nasitisha likizo zote,kwa Wakuu wa wilaya ,Wakurugenzi na wakuu wote wa idara ili mambo haya yaweze kutekelezwa,tumesema Hapa ni kazi tu”aliongeza Makala.

Alisema utekelezaji wa agizo la rais la kufanya usafi siku ya sikuu ya Uhuru inayofanyika Desemba 9 kila mwaka ,mapambano ya ugonjwa hatari wa Kipindupindu ambao umeendelea kusambaa sehemu kubwa ya nchi hayawezi kusubiri hadi watusmishi wa serikali watoke likizo.

Mkuu wa mkoa wa Kilimajaro,Amosi Makala akizunumza na wakuu wa wilaya ,wakurugenzi,Wakuu wa taasisi mbalimbali za umma katika kikao cha utendaji kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya mkuu wa mkoa. 
Wakuu wa wilaya za mkoa wa Kilimanjaro wakiwa katika kikao hicho,kutoka kuslia ni Mkuu wa wilaya ya Hai,Anthony Mtaka, Helman Kapufi (Mkuu wa wilaya ya Same) Novautus Makunga (Mkuu wa wilaya ya Moshi) na Lembris Kipuyo (Mkuu wa wilaya ya Rombo). 
Baadhi ya wakurugenzi wakiwa katika kikao hicho. 


Watendaji wengine wa serikali wakifuatilia hotuba ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro alipokutana nao . 
NA Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii kanda ya kaskazini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...