Ukiachana na hifadhi za taifa zitakazokufanya usichoke kutembelea miji na mikoa mbali mbali ndani ya Tanzania, ni uwepo wa hoteli za kifahari zenye utofauti wa kipekee na hoteli za nchi nyingine.
Jovago Tanzania, wadau wanaohusika na masuala ya Hoteli kimataifa, wanapenda kukuorodheshea tano bora ya hoteli zilizo kwenye chati ya kukupa mandhari zuri ya kiutalii wa kifahari hapa Tanzania.
Manta Resort-Pemba: Ni
hoteli ya kipekee yenye chumba cha kulala chini ya bahari ya Hindi. Hoteli hii
inakupa mandhari ya peponi utakapo jaribu kukaa ndani ya chumba hicho, hii ni
moja ya utalii ambao hutaweza kuusahau utembeleapo eneo hili kisiwani Pemba.
Essque Zalu Zanzibar: Essque Zalu ipo
Zanzibar, ni hoteli bora ya kimataifa yenye viwango vya huduma kwa hali ya juu
(five star). Ni sehemu pekee itakayokupa historia nzima ya Zanzibar na fursa ya
kutembelea fukwe kubwa nzuri zinazopatikana maeneo ya Nungwi. Imejengwa kwa nakshi za
kishwahili na za kisasa za kuvutia.
1 Singita sasakwa Lodge –Serengeti: Eneo lake ni
zaidi ya ekari 300,000. Hoteli inavyumba vilivyojengwa kwa mandhari ya
kitamaduni za kiafrika, na uwezo wa kuona madhari ya hifadhi ya taifa na mbuga ya
wanyama Serengeti.
1 Park Hyatt –Zanzibar:
Ni
hoteli inayokupa mandhari kamili na historia ya Zanzibar, hoteli imezungukwa na
bahari ya Hindi katika eneo la
kihistoria la Stone town.
Hyatt Regency- Dar es Salaam:Hii ni hoteli
yenye kiwango cha juu cha ubora wa kimataifa (Five star), ina uwezo wa kubeba
watu wengi zaidi ya hoteli yoyote Dar es Salaam. Ina mandhari nzuri ya bahari ya
Hindi, na vyumba vilivyojengwa kwa teknolojia ya hali ya juu, inafaa zaidi kwa
masuala ya makazi kwa mikutano ya kibiashara pia inakupa fursa ya
kutembelea sehemu tofauti tofauti
zilizo katikati ya mji wa Dar es salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...