Mdau Edwini Mjwahuzi ambaye ni Mpiga picha wa Magazeti ya Kampuni ya Mwananchi, jioni ya leo ameamua kuvunja kibanda cha Makapera na kukimbilia kwenye Mjengo wa wanandoa, kwa kufunga pingu za maisha na Bi. Hildegarda Mashauri kwenye Kanisa la Mtakatifu Joseph, Jijini Dar es salaam.
  Mdau Edwini Mjwahuzi na Mkewe Bi. Hildegarda Mashauri pamoja na Wasimamizi wao wakiwa kwenye ibada ya ndoa, iliyofanyika jioni ya leo kwenye Kanisa la Mtakatifu Joseph, Jijini Dar es salaam.
Mdau Edwini Mjwahuzi akimvisha pete Mkewe Bi. Hildegarda Mashauri, wakati wa Ibada ya Ndoa yao iliyofanyika kwenye Kanisa la Mtakatifu Joseph, Jijini Dar es salaam leo.
 Mdau Edwini Mjwahuzi na Mkewe Bi. Hildegarda Mashauri wakiwa ni wenye furaha tele mara baada ya kufunga pingu za maisha na kuwa mwili mmoja, kwenye Kanisa la Mtakatifu Joseph, Jijini Dar es salaam leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hongera na pongezi kwa hatua mliyoifikia Edwin na Hilda.. Mwenyezi Mungu awaongoze na kuisimamia ndoa na familia yenu mliyoianzisha..!

    ReplyDelete
  2. Hongera sana Edwin Mwenyezi MUNGU aibariki ndoa yenu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...