Ndugu na jamaa wanatarifiwa kwamba Bw. Hemed Mzee Ibrahim "Njemba" (pichani)  ametoweka nyumbani kwake Magomeni Makuti mtaa wa Mchinga namba 22 jijini Dar es salam toka siku ya Alhamisi tarehe 24/12/2015 na hadi hii leo Jumapili 27/12/2015 bado hajaonekana. 
Mzee Njemba alionekana kwa mara ya mwisho kwenye msikiti wa Magomeni Makuti muda wa alasiri alipokwenda kuswali, akiwa kavaa balaghashia (kama hiyo pichani), shati la light purple, suruali ya bluu na kandambili za bluu. Baada ya hapo hakurudi nyumbani kwake na hadi sasa hajulikani alipo. Mzee Njemba hupendelea kutembelea Magomeni Makuti.
Wanafamilia wanaomba mwananchi atayebahatika kumuona atoe tarifa kwa mkwewe Yusuf  anayepatikana katika namba 0784 606 262.
Wanatanguliza Shukurani za dhati kwa wote na kumuombea salama mzee wao.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Ms RMSangiwaDecember 26, 2015

    Insha'allah Allah atamrudisha SALAMA kwa njia ambayo ALLAH anaijua, naitakia SUBRA familia yake katika wakati huu mgumu. Sisi ndugu, jamaa na marafiki tuzidi kumuombea aliyepotea arejee salama na pia familia iwe na SUBRA. Amin

    ReplyDelete
  2. Wanawake wakati mwengine hukera majumbani hufanya wanaume kukimbia majumbani
    Inshaallah arudi nyumbani salama

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...