Ndugu na jamaa
wanatarifiwa kwamba Bw. Hemed Mzee Ibrahim "Njemba" (pichani) ametoweka nyumbani kwake
Magomeni Makuti mtaa wa Mchinga namba 22 jijini Dar es salam toka siku ya
Alhamisi tarehe 24/12/2015 na hadi hii leo Jumapili 27/12/2015 bado hajaonekana.
Mzee Njemba alionekana kwa mara ya mwisho
kwenye msikiti wa Magomeni Makuti muda wa alasiri alipokwenda kuswali, akiwa
kavaa balaghashia (kama hiyo pichani), shati la light purple, suruali ya bluu
na kandambili za bluu. Baada ya hapo hakurudi nyumbani kwake na hadi sasa
hajulikani alipo. Mzee Njemba hupendelea kutembelea Magomeni Makuti.
Wanafamilia wanaomba
mwananchi atayebahatika kumuona atoe tarifa kwa mkwewe Yusuf anayepatikana katika namba 0784 606 262.
Wanatanguliza Shukurani za
dhati kwa wote na kumuombea salama mzee wao.
Insha'allah Allah atamrudisha SALAMA kwa njia ambayo ALLAH anaijua, naitakia SUBRA familia yake katika wakati huu mgumu. Sisi ndugu, jamaa na marafiki tuzidi kumuombea aliyepotea arejee salama na pia familia iwe na SUBRA. Amin
ReplyDeleteWanawake wakati mwengine hukera majumbani hufanya wanaume kukimbia majumbani
ReplyDeleteInshaallah arudi nyumbani salama