Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Michael Mhando ameelezea kuridhishwa na matumizi ya mkopo uliotolewa na Mfuko huo kwa Hospitali ya mkao wa Singida.
Hospitali hiyo ilichukua mkopo wa Shilingi Milioni Mia Tano kutoka NHIF kwa ajili ya Ununuzi wa vifaa Tiba vya hospitali hiyo.
Akizungumza baada ya kukagua vifaa hivyo, Mhando amesema ameridhiswa na matumizi ya mkopo huo kwani umefanya kazi iliyokusudiwa.
Amesema NHIF itaendelea kushirikiana na uongozi wa mkoa huo ili kuboresha huduma za matibabu kwa wanachama wa NHIF na wananchi kwa ujumla.
Aidha amewahimiza watoa huduma wengine kuendelea kuchukua mikopo ili kuboresha huduma katika vituo vyao vya matibabu.
Hivi sasa Mfuko huo umeanza pia kutoa mikopo ya dawa ili kukabiiliana na uhaba wa dawa ktk vituo vya matibabu.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF ), Michael Mhando akikagua baadhi ya vifaa Tiba vilivyopo kwenye Hospitali ya mkao wa Singida, ambavyo ni Ultra sound, incubator, mashine ya dawa za usingizi, vitanda vya kujifungulia na kadhalika vilivyotolewa kwa mkopo na Mfuko huo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF )Bwana Michael Mhando akitoa maelekezo kwa Kaimu Mganga Mkuu wa Mkao wa Singida Dokta Ernest Mugeta (hayupo pichani) juu ya utumiaji wa vifaa hivyo, katika Mkoa wa Singida.
Baba nakuona. Kasi ya Magufuli inakufaa...
ReplyDelete