Baadhi ya waraghabishi wa kijiji cha Nyandekwa Wilayani Kahama wakiongea na waandishi wa habari waliofika kijijini hapo kwa ajili ya kujionea matokeo mbali mbali baada ya waraghabishi kuwasaidia wananchi hao kuchukua hatua katika kila jambo kwa maendeleo ya kijiji chao.
Mdau Krantz Mwantepele akihoji maswali kwa Dada Miriam Stefano (Aliyejishika tama ) ambaye amekuwa mchango mkubwa kwa kutoa elimu ya uzazi na mabadilko ya mwili kwa vijana wa kike katika baadhi ya shule za sekondari na msingi katika kijiji hicho.
Picha ya pamoja nikiwa na waraghabishi wa kijiji cha Nyandekwa Wilayani na waandishi wa habari tuliopata bahati ya kutembelea kijiji hicho na kujifunza namna gani wameweza kuwa chachu ya maendeleo katika kijiji hicho.
Na Krantz Mwantepele ,KAHAMA
Mkutano mkuu wa Kijiji cha Nyandekwa wilayani Kahama mkoani Shinyanga uliofanyika mwishoni wa mwezi wa tisa umeazimia kuwashikinikiza wazazi wa kijiji hicho kuwapeleka watoto wao shule Azimio hilo Pia limeelekezwa kwa vijana wanaokaa vijiweni kuwataka kushirki katika shughuli mbalimbali za kiuchumi na sio kukaa vijiweni pia kushiriki katika mikutano mbali mbali ya kijiji kujua maendeleo ya kijiji Iikihusisha mapato na matumizi.
Mkutano huo umepitisha maazimio matano yanayolenga kurejesha nidhamu Na heshima kijijini Nyandekwa hatua hiyo imefikiwa Kutokana Na wananchi wa kijiji hiki kutoona umuhimu wao kuchukua hatua za kujikwamua kiuchumi na pia Kuwa na ujasiri wa kuhoji mapato na matumizi kwa ajili ya kijiji chao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...