Ikiwa ni siku chache baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi wa Nchi Wanachama COP21 uliokuwa ukifanyika Paris, Ufaransa, ambao ulimalizika kwa kupitisha mkataba mpya wa mabadiliko ya tabianchi (Paris Agreement), wadau mbalimbali wamekutana kujadili matokeo ya mkutano huo.
Mkutano huo wa wadau umeandaliwa na ForumCC kwa kushirikiana na Rosa Luxemburg Stiftung (RLS) kwa lengo la kuangalia mazidi na mapungufu ya mkataba huo ambao umeweka historia mpya ya kuelekea juhudi za kupunguza ongezeko la joto duniani, kukabiliana na kupunguza madhara ya mabadiliko ya tabianchi.
Miongoni mwa vipengele vya mkataba huo vilivyojadiliwa na wadau hao ni pamoja na Kiwango cha nyuzi joto, Upunguzaji wa gesi Joto, Kukabiliana na mabadiliko ya tabainchi, Uharibifu na upotevu, Fedha za mabadiliko ya tabianchi, Mfumo wa taasisi na ushiriki wa serikali, waandishi wa habari pamoja na asasi za kiraia kwenye kuleta mchango wa makubaliano ya mkataba huo.
Picha ya pamoja ya Wadau hao
Mwakilishi wa ForumCC, Adam Athony akitoa mrejesho wa kilichojiri kwenye Mkutano wa Mbadailiko ya Tabianchi COP21 uliofanyika Paris, Ufaransa.
Mwakilishi wa Rosa Luxemburg Stiftung (RLS) Afrika Mashariki, Musa Bulegeya (katikati) akizungumza jambo wakati wa mkutano huo, kulia kwake ni Meneja Miradi ForumCC Rebecca Muna, wakati kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya ForumCC Yunista Kibona.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...