Rais wa Shirikisho la Filamu Simon Mwakifamba akiongea na vyombo vya habari wakati wa uzinduzi filamu ya ‘Going Bongo’ uliofanyika katika ukumbi wa cimema wa Cinemax jana Ijumaa jijini Dar es salaam

WADAU mbalimbali waliofika kwenye onyesho la kwanza la filamu ya Mtanzania anayeishi nchini Marekani wametoa sifa kemkema kuhusu filamu hiyo inayokwenda kwa jina la ‘Going Bongo’ na wamewataka wasanii wa hapa nchini waige mfano wake.

Wakizungumza baada ya kutoka kuaitazama ndani ya ukumbi wa cimema wa Cinemax Ijumaa usiku mkongwe katika filamu Ibrahimu Banane almaarufu kwa jina la ‘Mzee Katembo’ alisema kwamba mtunzi wa filamu hiyo amewashtua wasanii wa hapa nyumbani na Afrika Mashariki kwa ujumla.

“Ametushtua sisi kwamba tutunge filamu na kuzicheza katika kiwango cha kimataifa na tuchukue muda mrefu ili kuweza kutunga na kurekodi filamu zetu kama tunataka kulikamata soko hilo na kujitangaza kwa ujumla endapo tu tutafuata nyayo za mtunzi wake Ernest Napoleon.” alisema Katembo.

Alisema m ameiangalia filamu hiyo inayokwenda kwa jina la ‘Going Bongo’ ni nzuri kila muigizaji amesimama katika nafasi yake na kuuvaa uhusika vilivyo na endapo wasanii wa hapa nyumbani watataka kutengeneza filamu nzuri wasiogope kuingia gharama kama jinsi filamu hiyo inavyoonesha muandaaji alivyoingia gharama kwamba aimerekodiwa katika nchi mbili tofauti.

“Hapa nyumbani sisi tumezoea kuona kwamba msanii anafyatua filamu mbili ndani ya mwezi mmoja jambo ambalo hupunguza ubunifu kwani ni vigumu kichwa kimoja kuweza kutoa kitu kizuri ndani ya mwezi mmoja” alisema Katembo.

Msemaji wa Waigizaji nchini Massoud Kaftani aliimwagia sifa filamu hiyo na kusema kwamba wamepata somo kutoka kwa Ernest hivyo wanashukuru pia kwa kupata nafasi ya kuishuhudia filamu hiyo na kuahidi wkamba watafanyia kazi changamoto mbalimbali zilizo ndani ya tasnia ya filamu na maigizo nchini.

Wakati huohuo Rais wa Shirikisho la Filamu Simon Mwakifamba aliongeza kwa kusema kuwa yeye binafsi amevutiwa na filamu hiyo kutokana na kuzingatiwa kwa vina na mpangilio mzuri, “hili ni jambo la kujivunia kama watanzania pia tunatoa wito kwa watanzania wengine wanao ishi nje ya nchi kujipanga na kuibua vipaji vyao kimataifa kama jinsi alivyotuonesha Ernest hivyo huko waliko nina imani na wao wameifuatilia filamu hii ya Going Bongo ilete chachu kwa watanzania wanaoishi ughaibuni na wa hapa nyumbani wote tujipange kwa pamoja katika kuikuza na kuiendeleza tasnia hii” alisema Mwakifamba.

Filamu hiyo ilishuhudiwa na wadau mbalimbali akiwamo Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ huku akiitoa maneno ya kuisifa gfilamu hiyo na kusema kuwa muandaaji ametoa somo kwa wasanii wahapa nchini.

Filamu hiyo inayokwenda kwa jina la ‘Going Bongo’ ilioneshwa kwa mara ya kwanza kwenye ukumbi wa sinema wa Century Cinemax uliopo Mlimani City, Jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na mashabiki wengi ambao wengi wao walikiri kuvutiwa nayo.

Filamu hiyo ambayo mpaka sasa imetwaa tunzo kadhaa, pamoja na tunzo ya Ziff ina maudhui ambayo yanonyesha maisha ya Daktari aliyejitolea kwenda kufanya huduma nchini Tanzania kwa muda wa mwezi mmoja huku mtunzi na muandishi pia aliyeisimamia katika kuitengeneza na kuigiza filamu hiyo ni Ernest Napoleon .

Filamu hii imerekodiwa majiji makubwa mawili ambayo ni Dar es Salaam na California Marekani, inaelezea sehemu ya maisha ya kweli aliyonayo Daktari mwenye asili ya nchini Ufaransa aliyeondoka Ulaya na kwenda kufanya kazi barani Afrika.


Kati ya tuzo ambazo filamu hii imeshinda ni pamoja na, Filamu Bora Afrika Mashiriki katika tamasha la Zanzibar International Film Festival (Ziff) na Filamu Bora ya Kimataifa katika tamasha la ‘Black Entertainment Fashion’, ‘Film and Television Awards’ (BEFTA)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...