

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (aliyevaa tai) akiwasalimia wananchi wanaosubiri kupata huduma ya Hati za Kusafiria katika Ofisi za Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam. Waziri Kitwanga alifanya ziara ya kikazi katika ofisi hizo kwa lengo la kujifunza kazi mbalimbali zinazofanywa na Uhamiaji. Katika hotuba yake, licha ya maelekezo mengine aliyoyatoa kwa viongozi wakuu, pia aliitaka Idara hiyo ya Uhamiaji kuanza rasmi kwa operesheni ya kuwakamata Wahamiaji Haramu nchini. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Afisa Uhamiaji anayeshughulika na uchapaji wa Hati za Kusafiria, Amir Hassan (kushoto), akitoa maelezo ya jinsi wanavyozichapisha Hati za Kusafiria, kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) ambaye alifanya ziara ya kikazi katika ofisi za Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile (kushoto) akiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga, wakati Waziri huyo alipokuwa anafanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na Uhamiaji. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akiwaeleza jambo Watendaji Wakuu wa Idara ya Uhamiaji wakati alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya idara hiyo, Kurasini, jijini Dar es Salaam leo. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) wakati Waziri huyo alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (wasita kulia), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil (watano kushoto), Naibu Katibu Mkuu, John Mngodo (wanne kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi Wakuu wa Idara ya Uhamiaji wakati Waziri huyo alipotembelea Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam. Wasita kushoto ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mheshimiwa Waziri Kitwanga;
ReplyDeleteAnza kazi yako kwakasi nzuri. Tunakupongeza na pia ninakuombea baraka tele. Mheshimiwa hapo ulipotembelea Idara ya Uhamiaji Makao Makuu kuna balaa la joto na kutokuwa na hewa yakutosha hasa upande wa wanaohudumiwa. Uendapo hapo huwa wanazima AC na au wanalengesha upande walio watendaji tu. Ni ukweli Mheshimiwa wateja tunapata adha kuu na tafrani tuendapo kupata huduma hapo.Kama haiwezekani kuwasha hizo AC basi wabadilishe mpangilio wa ofisi hizo na kutufungulia madirisha zaidi, ili hewa iwe safi na yakutosha. Tunaomba haya kwako wewe Mheshimiwa Waziri na hata watendaji wako wengine. Ni balaa la afya Mheshimiwa kwani madhara na athari zaweza zisionekane leo lakini siku moja zitakuja. Nadhani AC hizo zililengwa kwa kila atumiaye jengo hilo na si wafanyao kazi tu waliopo kwenye vizimba vya vioo vilivyojaa baridi na hewa safi. Tafadhali tunaomba kwako kama Watanzania na wengine watumiao ofisi hizo. Mungu ibariki Tanzania, Viongozi na watu wake wote.
Mrs B.S-Kibondo