Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Charles Kitwanga akizungumza na mahabusu na wafungwa waliopo Gereza la Wanawake Segerea, jijini Dar es Salaam alipofanya ziara katika Gereza hilo kujifunza shughuli mbalimbali za uendeshaji wa Magereza. Kulia kwake ni Waziri wa Sheria na Katiba, Dkt. Harrison Mwakyembe. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil, Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria na Katiba, Maimuna Tarishi. Wapili kulia ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, CGP John Minja.
Waziri wa Sheria na Katiba, Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akiangalia bidhaa zinazotengenezwa na wafungwa wa kike wa Gereza la Wanawake Segerea ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa program ya urekebishaji magerezani. Pembeni yake ni Mkuu wa Gereza Kuu Segerea, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Abdalah Kiangi. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe Charles Kitwanga na Waziri wa Sheria na Katiba, Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) wakitoka Gereza la Wanawake Segerea baada ya kuzungumza na Mahabusu na Wafungwa wa Gereza hilo lililopo jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...