Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akizungumza na mmoja wa
wakina mama anayemhudumia mwanae katika wodi ya watoto Hospitali ya
rufaa ya Bombo mkoani Tanga alipofanya ziara ya kushtukiza leo mchana
Disemba 20, 2015.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akimsikiliza mmoja wa
akina mama aliyelazwa kwenye wodi ya wazazi wakati wa ziara ya
kushtikiza aliyoifanya mchana wa leo Desemba 20, 2015 katika Hospitali
ya rufaa ya Bombo mkoani Tanga.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akizungumza na mmoja wa
wahudumu wa afya (jina lake halikuweza kupatikana kiurahisi) wa dirisha
la dawa katika Hospitali ya rufaa ya Bombo mkoani Tanga alipofanya ziara
ya kushtukiza mchana wa leo Disemba 20, 2015.
Daktari aliyekuwa kwenye
mafunzo, Dkt. Zuberi (Medical Intern) akitoa maelezo ya namna
wanavyohudumia wananchi wanaofika hospitalini hapo Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu (kulia)
aliyefanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya rufaa ya Bombo,
mkoani Tanga mchana wa leo Desemba 20, 2015 ambapo Waziri huyo alikutana
na changamoto utoro wa madktari wa zamu kutokuwepo kwenye kituo chao
cha kazi katika Hospitali ya rufaa ya Bombo, mkoani Tanga.
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa
Tanga (RMO), Dkt. Clement Marceli akimwelezea changamoto wanazokabiliana
nazo katika Hospitali ya rufaa ya Bombo mkoani Tanga Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu (hayupo
pichani).
Baadhi ya madaktari waliokuwa
mafunzoni wakizungumza na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu aliyefanya ziara ya kushtukiza
katika Hospitali ya Rufaa ya Bombo, mkoani Tanga mchana wa leo Disemba
20, 2015.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akipitia orodha ya
mahudhurio ya zamu za Madaktari na Wauguzi ambao wengi hawakuwepo kazini
wakati wa ziara yake ya kushtukiza katika Hospitali ya rufaa ya Bombo,
mkoani Tanga aliyoifanya leo mchana Disemba 20, 2015.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...