TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, amemteua Ndugu Julian Banzi  RAPHAEL (pichani) kuwa Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania.
Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue imeeleza kuwa uteuzi huo umeanzia tarehe 26 Januari, 2016.
Kabla ya uteuzi huu Ndugu Julian Banzi RAPHAEL alikuwa Katibu mkuu, Wizara ya Biashara na Viwanda, Serikali ya Mapinduzi  Zanzib ar. 
Ndugu Julian Banzi RAPHAEL anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Ndugu Juma RELI ambaye muda wake umemalizika tarehe 12 Julai, 2015.

Gerson P. Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU,
DAR ES SALAAM.

28/01/2016

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...