SHIRIKA LA VIWANGO TANZANIA (TBS), LINAPENDA KUWAKUMBUSHA WAUZAJI WOTE WA BIDHAA ZA MATAIRI YALIYOTUMIKA, NGUO ZA NDANI ZA MITUMBA, VILAINISHI VYA MAGARI NA MITAMBO
(OIL LUBRICANTS) NA BIDHAA ZOTE  AMBAZO HAZIJATHIBITISHWA UBORA WAKE NA TBS, KUZIONDOA SOKONI BIDHAA HIZO MARA MOJA. 

HATUA KALI ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA KWA YEYOTE ATAKAYEKAIDI AGIZO HILI.


TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA MKURUGENZI MKUU WA   SHIRIKA LA VIWANGO TANZANIA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. MIMI NI ASKARI WA TPDF NAKAA PUGU-DUNDA NYINYI WATU WA TBS,NJOONI HAPA KAMATA PUNDA HAPA PUGU WAPO ZAIDI YA MIA HIVI ,WATU WAKO WANATOA VIBALI VYA MAGENDO KUSAFIRISHA PUNDA WA KUCHINJA KUTOKA SINGIDA NA DODOMA KULETA DAR ES SALAAM ILI WACHINJE KWENDA CHINA,WALE PUNDA WALIOKATALIWA DODOMA WACHINA WAMEHAMISHIA PUGU-DUNDA KATIKA MACHINJIO YASIYO RASMI,INAWEZA KUWA HATARI HII NYAMA WAKATUCHANGANYIA NA YA NG'OMBE KAMA DODOMA JE SHERIA ZA VIWANGO ZINARUHUSU MACHINJIO YA PUNDA KUWA JIRANI NA MAKAZI YA WATU????

    ReplyDelete
    Replies
    1. Heko kamanda kwa kuwa na uchungu na nchi yako na wananchi wake.

      Delete
  2. WEWE ASKARI SIJUI TPDF SIJUI NINI KWANI KITU GANI KISICHOLIWA HAPA DUNIANI? PUNDA NI SAWA NA NGOMBE TU KAMA HUJUI , WENZETU WEST AFRICA WANAKULA PAKA SOKWE,MBWA,, HAPA HAPA TANZANIA MACHINGA HUKO WANAKULA PANYA MBONA HAWAPAKEMEWA NA MTU.

    SKUUNGI MKONO KWA HULO,.

    SISI MBONA TUNAKULA NYAMA YA NGOMBE NA INDIA NI MARUFUKU KULA NGOMBE HILO UNALIFAHAMU

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sasa hata kama wanakula vyote hivyo ulivyovita sasa ndio na wengine wale? Ukiambiwa kula mavi utakula? Si kwa sababu umesikia wengine wanakula

      Delete
  3. MJESHI UPO SAHIHI JE WAKIUZIWA NYAMA YA MBWA WASILALAMIKE,USHAURI WANGU KWAKO MJESHI WAITE NEMC HAWA NI WATU WA MAZINGIRA.KUJUA HAYO MACHINJIO NI RASMI KWA UCHINJAJI?? NA JE HAO PUNDA WANA VIBALI HALALI VYA WIZARA YA KILIMO NA VETERNARY??

    ReplyDelete
  4. TBS (na wakaguzi wengine) wana kazi kubwa sana. Madukani kuna vitu takribani asilimia 40 havifai kwa matumizi ya binadamu, ukaguzi ukisimamiwa vizuri itakuwa balaa, vyakula (na ma-apple barabarani), simu zisizo na viwango, vipodozi, mbegu, mbolea, hata dawa za mifugo na za binadamu, malori-basi yanayobeba abiria, n.k.

    Nakumbuka siku moja nikiwa mitaani ughaibuni, ghafla wahusika wakaingia duka moja, kumbe ni surprise inspection ya kukagua bidhaa zisizofaa!! Hapa kwetu nilikoishi miaka takribani 50 (35 kati ya hiyo nikiwa utambuzi kamili) sijawahi kukutana na surprise visits kama hizo, hivyo tunauana wenyewe taratibu!!

    Hivi tumelala usingizi kiasi hicho?!

    ReplyDelete
  5. MIMI MWANAJESHI WA JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA -TPDF,KAMA NILIVYOJIELEZA KAMA MCHANGIA MADA NAMBA MOJA NA NINAISHI KARIBU NA ENEO HILI AMBALO PUNDA HAWA WAPO.KWA KWELI INASIKITISHA HASA KUONA NCHI INAJIENDEA KAMA HAINA MWENYEWE.JE NI SAHIHI MACHINJIO TENA YA PUNDA TUNAOWATUMIA KUBEBA NA KUSAFIRISHA VITU,KUWEKWA KATIKA MAZINGIRA AMBAYO SI MAZURI? KWA HABARI NILIONAZO HIVI SASA WAKATI WANAENDELEA NA HUO UJENZI WA MACHINJIO HAYO HAO 100 WALIOPO HAWANA CHAKULA CHA KUTOSHA WANAKUFA.WANAOKUFA WANACHUNA NGOZI NA MIILI YAO INAFUKIWA KIENYEJI TU.NI BIASHARA AMBAYO INAONEKANA INAFANYWA KAMA KUFICHWA SASA SIJUI HAWA WAKUBWA WA TBS,MALIASILI,KILIMO,MAZINGIRA,NA HALMASHAURI YA JIJI HAWAONI KAMA KUNA MAPATO YANAPOTEA KWA KUWA HAKUNA USHURU UNAOLIPWA.NINAAMINI KUTOCHUKULIWA HATUA ZA HARAKA NI DALILI TOSHA KUWA NCHI HII ITAENDELEA KUWA MASIKINI WA KUTOAFUATA TARATIBU ZA KUKUSANYA MAPATO NAKADHALIKA

    ReplyDelete
  6. Mwanajeshi wa TPDF, nakushauri nenda ofisi husika katoe taarifa nina uhakika watafuatilia, sometimes ku post humu haisaidii

    ReplyDelete
  7. Msoja safi hawa wachina wamezidi wanafanya tz ni shamba la bibi.

    Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  8. Hivi VIROBA vina ubora wa TBS? Vinaathiri sana nguvu kazi ya Taifa letu!Kwa nini visiteketezwe? Ufungaji wake unakuwa rahisi kuficha na kutumika wakati wowote. Ajali zinachangiwa na viroba pia.

    ReplyDelete
  9. Viroba vina ubora wa TBS?

    ReplyDelete
  10. Habari. mtoa mada wa kwanza afisa wa jeshi letu la Ulinzi. naomba tuwasiliane nahitaji kufuatilia hiloi suala kwa kina zaidi. mawasiliano yangu hayo 0719076376 au email chalefamily@yahoo.com

    plz tuwasiliane.

    ReplyDelete
  11. JE UMESIKILIZA REDIO CLOUDS LEO???? 25 JANUARY 2016 KUHUSU HAO PUNDA????

    ReplyDelete
  12. Mhe.Makamba nimefurahi kusikia kuwa umewasimamisha kazi watu wa NEMC kwa kutoa kibali kwa wachina hawa kuchinja punda huko Dodoma,kwa taarifa yako hao punda wameletwa Dar na wapo Pugu wamefichwa kama mia kuna machinjio ya siri yanaandaliwa na kibaya zaidi wachovu wanachinja wanauza nyama kinyemela.nina uhakika watu wa Pugu Mwakanga,Dunda na Kigogo fresh wawe makini vinginevyo wanakula mishikaki ya punda.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...