Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Hamad Yussuf Masauni akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu hatua zinazochukuliwa na Wizara kudhibiti wageni wanaoishi nchini na kufanya kazi kinyume na sheria. Mkutano huo ulifanyika Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam.
Afisa Uhamiaji mkoa wa Dar es Salaam, Naibu Kamishna, Johannes Msumule akizungumza katika mkutano na Waandishi wa Habari ambapo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Hamad Yussuf Masauni alizungumzia hatua zinazochukuliwa na Wizara kudhibiti wageni wanaoishi na kufanya kazi nchini kinyume na sheria. Mkutano huo ulifanyika Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam.

Sehemu ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Hamad Yussuf Masauni, wakati wa mkutano wa kuzungumzia hatua zinazochukuliwa na Wizara kudhibiti wageni wanaoishi nchini na kufanya kazi kinyume na sheria. Mkutano huo ulifanyika Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi jijini Dar es Salaam.
(PICHA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI – WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. The mdudu, kwenye hii wizara sijawahi kusikia MAJIPU YOYOTE YAKITUMBULIWA yaani kama vile ilikua safi wakati ilikua na ubaba ishaji usio semekana tunataka kuona Mijipu inatumbuliwa hatutaki mchezo na #MAFISADI

    ReplyDelete
  2. Mie naona hapa kuna tatizo kubwa hili ni jipu ambalo yabidi Rais mwenyewe alitumbue au Mr.Majaliwa. Hebu tujiulize maswali kadhaa ya msingi juu ya swala la Wageni kuchukua nafasi za kazi za wazawa.
    1.Mbona kila kukicha ni ufuatiliaji wa vibali,wakati kila kitu kiko wazi,Waziri Muhagama alitoa waraka wa vibali kuwasilishwa ndani ya siku 14,zilipokwisha akaja na ngonjera ya kuunda kikosi kazi,wakati hajatuambia ni kampuni ngani zimetii amri,ili kikosi kazi kiende kwa zile ambazo hazijatimiza.
    2.Hapa pia tunaona mgongano wa amri toka kwa mawaziri-masauni,Mavunde na muhagama,swala kuu hapa ni wafanyakazi wa kigeni,iweje kila kukicha inatoka amri mpya utafikiri jesheni.hebu hawa watu wakae pamoja na kutueleza jambo moja la uhakika na si ubabaishaji wa kutumia media wakati utelkelezaji ni sifuri.Mie naona imefika wakati wa Mawaziri kukutana kuweka mkakati wa kutatua swala hilki na kuwawajibisha wale wote waliohusika na utoaji vibali na si vinginevyo.Kwani Kamishna wa TRA,Mkurungezi wa TRC na Takukuru wao hawakua na haki ya kuundiwa kikosi kazi cha kutatua changamoto za idara zao??hebu tuwe fair,twaomba makamishina wote wajiuzulu na kuacha watu wengine watuondolee hawa makanjanja

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...