Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya mafunzo ya ufundi stadi (VETA), Geofrey Sabuni akizungumza na wahitimu wa mafunzo ya muda mfupi katika chuo hicho leo jijini Dar es Salaam.
Katika mahafali hayo wamezawadiwa vyeti vya kufunzu masomo yao katika chuo cha mafunzo ya ufundi leo jijini Dar es Salaam.
Viongozi wa chuo wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wahitimu leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

Na Chalila Kibuda wa Globu ya Jamii.
WAHITIMU 67 wasio katika Mfumo Rasmi watunukiwa vyeti katika kuwarasimisha katika ujuzi waliopata  katika maeneo yao ya kazi.

Akizungumza katika mahafali hayo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mafunzo na Ufundi Stadi (VETA),Geofrey Sabuni amesema kuwa wataendelea kutoa mafunzo hayo ili kuwatambua mafundi wa mitaani ambao wamekuwa hatambuliki kutokana na kukosa mafanzo katika taasisi zinazotambulika.

Amesema kuwa nia ya kuwafikia watu 5000 katika kurasimisha kazi wanazozifanya kutokana na mchango mkubwa wa taifa huku wakiwa hawatambuliki.

Sabuni amesema kuwa VETA itahakikisha inaendelea kutoa mafunzo kwa vijana katika ujuzi mbalimbali pamoja na wale ambao hawako katika mfumo rasmi kuwatambua.

Aidha amesema kuwa katika jitihada zote kuna changamoto hivyo kwa wahitimu lazima waendelee kuongeza ujunzi wa mafunzo ya muda mrefu  katika kuwa wabobezi huku wakiwa na vyeti vinavyoonyesha ujuzi.

Kaimu Mkuu wa Chuo cha Veta Dar es Salaam,Violet Fumbo amesema katika mafunzo wanayotoa wanatambulika sehemu zote kutokana na mafunzo hayo kuingizwa katika mitaala.

Violet amesema katika mambo wanayoyafanya ni kutaka vijana kujituma katika ujuzi waliofanya kazi hiyo 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...