Afisa Uhusiano wa Manispaa ya Ilala Bi Tabu Shaibu akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu mikakati ya Manispaa hiyo katika kukusanya Kodi ya majengo ikiwemo kuelimisha umma juu ya umuhimu wa kulipa kodi pasipo shuruti. Kushoto ni Meneja wa Kodi ya Majengo wa Manispaa hiyo Bw. Kasuja Revelian.
Meneja wa Kodi ya Majengo toka Manispaa ya Ilala Bw. Kasuja Revelian akifafanua kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu hatua zitakazochukuliwa na Serikali kwa wale wote watakaoshindwa kulipa kodi ya majengo kwa wakati ikiwemo kufikishwa katika vyombo vya sheria.Picha na Frank Mvungi.

WAMILIKI wa majengo katika Halmashauri ya Ilala wamehimizwa kulipa kodi ya majengo ili kufanikisha maendeleo ya nchi.

Hayo yamesemwa leo na Afisa Uhusiano wa Halmashauri ya Ilala Tabu Shaibu alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari  Jijini Dar es salaam, amesema kuwa wamiliki wa majengo wanapaswa kulipa kodi ndani ya siku 30 tangu anapokuwa amepewa hati ta madai.

Ameongeza kuwa hati hizi uanza kutolewa Julai ya kila mwaka na mlipa kodi anatakiwa kuwa amelipa ifikapo tarehe 31/10 kila mwaka ambapo baada ya mwaka mmoja mlipa kodi atatikwa kulipa faini ya asilimia 25 kwenye kiasi cha kodi ambacho hakijalipwa.

“Kulipa kodi ni lazima kwa maendeleo ya nchi na kodi hii hutozwa chini ya Sheria  ya mamlaka za miji (The Urban Authorities Act) namba 2 ya 1983 na marekebisho yake 2002.”. Alisema Tabu

Aidha Tabu Shaibu amesema wapo wafanyabiashara  wakubwa ambao bado wanadaiwa kodi ya majengo, miongoni mwao ni Air Tanzania Company Limited Tsh 14,124,081.00, Peacok Hotel Tsh 69,960,458.00, Mohamed Entreprises Limited Tsh 6,274,233.00, Business Printers tsh 6,561,870.00, lamada Hotel & Apartments limited Tsh 24,483,020.00 na Yusuph Mohamed Manji & Salim J Mussa Tsh 21,020,715.00.

Kodi ya majengo ni miongoni mwa vyanzo vikubwa  vya mapato katika Halmashauri, hivyo  ni wajibu wa kila mwananchi kulipa kodi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...