Na John Nditi, Morogoro 
 POLISI mkoani hapa leo imewatia mbaroni wahamiaji haramu 12 kutoka nchini Ethiopia pamoja na watanzania wawili katika eneo la Mikumi, barabara kuu ya Morogoro- Iringa. 
 Wahamiaji hao haramu walikamatwa usiku wa kuamkia Februari 2, mwaka huu majira ya saa nane na nusu usiku wakiwa katika gari lenye namba za usajili T 876 BHZ aina ya Toyota Noah , iliyokuwa ikiwndeshwa na Kimu Mustafa (25) mkazi wa Segera, mkoani Tanga akiwa na Kondakta wake aitwaye Rashid Ally (17) pia mkazi wa Segera Tanga. 
 Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Leonaerd Paulo, dereva wa gari na kondakta wake walieleza kuwa walielekezwa na tajiri wao kuwapakia wahamiaji haramu hao kutoka Mji wa Chalinze , mkoa wa Pwani. 
 Kamanda huyo alisema, kwa mujibu wa dereva huyo , kuwa tajiri wake alimpingia simu akiwa Segera na kumwelekeza kuwa aende Chalinze kuwachukua watu na kuwapeleka hadi Tunduma kwa vile walikuwa wakienda nchi ya Afrika Kusini. 
 Kamanda Paulo alisema kuwa uchunguzi wa awali umeonesha kuwa wahamiaji haramu hao walikuwa wanasafirishwa hadi Tunduma ili baadaye waelekee Afrika Kusini.
Amesema watuhumiwa hao wanaendelea kuhojiwa na kuwatafuta wafadhili wa biashara hiyo haramu na baada ya uchunguzi kukamilika watafikishwa Mahakamani.






   Gari walilokuwa wakitumia wahamiaji  haramu wa Ethiopia ( mbele ) waliokamatwa likiwa nje ya jengo la Kituo Kikuu cha Kati cha Polisi mjini Morogoro.
 Wahamiaji  haramu wa Ethiopia waliokamatwa na Polisi,  jana wakiwemo na watanzania wawili ,eneo la Mikumi, wilayani Kilosa  katika barabara kuu ya Mikumi- Iringa, wakiwa chini ya Ulinzi wa Polisi eneo la viwanja vya  Jengo la Kituo Kikuu cha Kati cha Polisi mjini Morogoro.
  Wahamiaji  haramu wa Ethiopia ( mbele ) waliokamatwa wakiwasili eneo la viwanja vya  Jengo la Kituo Kikuu cha Kati cha Polisi mjini Morogoro.
   Wahamiaji  haramu wa Ethiopia ( mbele ) waliokamatwa wakiwasili eneo la viwanja vya  Jengo la Kituo Kikuu cha Kati cha Polisi mjini Morogoro.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo, akielezea jambo kwa waandishi wa habari , mbele ya wahamiaji  haramu wa Ethiopia waliokamatwa usiku wa kuamkia Februari 2, mwaka huu  pamoja  na watanzania wawili eneo la Mikumi, wilayani Kilosa  katika barabara kuu ya Mikumi- Iringa,  baada ya kuwapatia mji wa Chalinze na kwenda nao Tunduma ili wavuke mpaka kuelekea Afrika Kusini. Picha na John Nditi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Warudisheni tu kwao, ni njaa tu imewaleta. Mzee Magufuli anapiga mabao ya mbali kimya kimya, amakweli hapa kazi tu

    ReplyDelete
  2. Let's be reasonable. We can do this exercise at less cost. If those immigrants were going out of country at their own cost why bother. Entering should be hard not leaving. Now you have to care for them. Be reasonable

    ReplyDelete
  3. Kwanza hawaelekei bongo. Wanaelekea zao South Africa. Bongo kwenyewe njaa kali nako. Wala hakuna tofauti na walikotoka. Hata huko South ni hivyo hivyo nako. Kwa hiyo wasiwanyanyase na wawape chakula ni halakati za mangaiko tu binadamu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...