Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasilisha bungeni Mapitio na Mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka 2016/2017.
UTANGULIZI
1.
Mheshimiwa Spika, naomba kutoa
Hoja kwamba kutokana na taarifa zilizowasilishwa leo katika Bunge lako Tukufu
na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria na Mwenyekiti wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI zilizochambua Bajeti ya Ofisi ya
Waziri Mkuu, Bunge lako sasa lipokee na kujadili
Taarifa ya Mapitio ya Utekelezaji wa Kazi za Serikali kwa Mwaka 2015/2016 na
Mwelekeo wa Kazi za Serikali kwa Mwaka 2016/2017. Vilevile, naliomba Bunge lako
Tukufu likubali kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya
Waziri Mkuu na Taasisi zilizo chini yake kwa mwaka 2016/2017.
2.
Mheshimiwa Spika, huu ni Mkutano wa Bunge wa kujadili Bajeti ya Serikali
baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwezi Oktoba, 2015. Hivyo naomba nitumie
fursa hii kuwashukuru Watanzania kwa kuendelea kuwa na imani na Chama Cha
Mapinduzi na hivyo kukiwezesha kushinda na kukipa tena ridhaa ya kuunda
Serikali na kuiongoza Nchi yetu. Aidha, kwa njia ya pekee napenda kumpongeza
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania kuongoza Serikali ya Awamu ya Tano. Pia, nampongeza
Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuchaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...