Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi akizungumza katika siku ya tatu ya Mkutano Maalum wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu mafanikio na changamoto za kukabiliana na tatizo la dawa za kulevya duniani.
Sehemu ya Washiriki wa Mkutano Maaluma wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu dawa za kulevya.
Balozi Tuvako Manongi ambaye aliongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huu akiwa na Bw. Rogers William Siyanga na Bw. Khamis Abdalla muda mfupi kabla ya kulihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lililokutana kujadili changamoto za dawa za kulevya. Mkutano huo umemalizika siku ya Alhamis.
Na Mwandishi Maalum, New York
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imesema, waathirika wa dawa haramu za kulevya wanatakiwa kusaidiwa badala ya kuwafunga jela.
Hayo yameelezwa jana ( Alhamis) na Balozi Tuvako Manongi, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, katika Mkutano Maalum wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa uliokuwa ukijadili mafanikio, juhudi na changamaoto za kukabiliana na tatizo la dawa za kulevya duniani.
Balozi Manongi ameongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano huu wa siku tatu na ambao umewashirikisha Viongozi Wakuu wa Nchi, Serikali na Mawaziri kutoka mataifa mbalimbali.
“Tunapoangalia mbele, mkazo wetu uwe katika kuhakikisha tunapunguza idadi ya watu wanaojihusisha na matumizi ya dawa haramu za kulevya na tunapunguza idadi ya watu wanaofariki kutokana na matumizi ya dawa hizo” akasema Balozi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...