· Mfumo wa kwanza wa mafunzo ya ufundi kwa njia ya mtandao Tanzania
· Kuleta ufarahisi na gharama nafuu
· Mafunzo kupatikana kupitia application maalum
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mpango wake wa kijamii wa Airtel FURSA imeshirikiana na Mamlaka ya elimu ya ufundi Tanzania (VETA) kuanzisha application mpya ijulikanayo kama “VSOMO” yaani VETA SOMO, ili kuwawezesha vijana kupata kozi mbalimbali zinazotolewa katika vituo vya VETA nchini kupitia simu za mkononi . Kuanzishwa kwa VSOMO itasaidia kupanua wigo wa mpango wa Airtel FURSA na kuwafikia vijana wengi zaidi nchini.
Akiongea kuhusu uhusiano huo, Mkurugenzi mkuu wa Airtel Sunil Colaso alisema” tumeona ni muhimu kuwekeza kwenye mpango huu wa VSOMO kwa kuwa tumeona vijana wengi wana kiu na haja ya kutaka kujifunza na kuhitimu mafunzo ili kukuza biashara zao na kupata taaluma zitakazowawezesha kujiajiri. Matumizi ya simu za kisasa yanakuwa kila siku, mpaka sasa takribani wateja milioni 10 wanatumia simu za kisasa na kati yao 70% ni vijana. Hivyo VSOMO itawafikia vijana wengi zaidi nchini kwa urahisi zaidi.Na ndio maana tunauza simu zetu kwa bei ndogo ya hadi Tshs elfu 80,000/=kuhamasisha mafunzi kwa kupitia njia ya simu za mkononi”.
“Tunaamini ushirikiano huu kati ya VETA na Airtel FURSA utawawezesha mamilioni ya vijana wakitanzania kupata mafunzo ya ufundi yanayotolewa na VETA wakati wowote na mahali popote kupitia simu zao za mkononi. Tunauhakika application hii ya VSOMO itachochea kukua kwa elimu kwa vijana wengi na kuwawezesha kuwa na wafanyabiashara na wafanyakazi bora walio na nyenzo zinazohitajika katika kuleta ufanisi”. Aliongeza Colaso
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Bwana Geoffrey G Sabuni alisema “ nafurahi kuwa sehemu ya utambulisho wa kihistoria wakuanzishwa kwa mafunzo ya ufundi kwa njia ya simu yenye lengo la kuwapatia watanzania nafasi ya kujiunga kwa wingi katika stadi za ufundi. Bwana Sabuni aliwapongeza timu nzima iliyoshiriki katika kuanzisha ubunifu huu wa VSOMO na kusema ni jambo litakalowezesha watanzania kwa mara ya kwanza katika historia ya ufundi stadi kuweza kuwa wataalamu watakaopeleka nchi katika uchumi wa kati. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA alisisitiza VSOMO inaendana na malengo ya VETA ya kuongeza idadi ya wanafunzi wanaojifunza mafunzo ya ufundi na hivyo kufanya vizuri kwa mafunzo haya kwa hatua hii ya awali kutapelekea kutanua wigo zaidi ili kufikia vijana wengi zaidi
Kwa upande wake Mkuu wa chuo Veta Kipawa, Eng. Lucius Luteganya alithibitisha kuwa Mafunzo kwa njia ya mtandao yamezoeleka sana duniani lakini kwa Tanzania hii ni mara ya kwanza kuanzishwa kwa mafunzo ya ufundi kwa njia ya mtandao. Kila mwaka VETA inapokea maombi ya kujiunga na kozi mbalimbali toka kwa vijana zaidi ya elfu 15 nchini na theluthi tatu ya maombi hayo ndo yanayokubaliwa na kupokelewa katika vituo vyetu nchini na kuacha theluthi mbili bila kupata fursa ya mafunzo. VSOMO kwa kiasi kikubwa kitaongeza uwezo wetu wa kufundisha watanzania wengi zaidi hususani vijana hivyo kuongeza idadi ya watu wenye ujuzi na kuchochea uchumi wa nchi kukua kwa kasi zaidi, alisema Luteganya
” ili kuhakikisha tunasimamia viwango vya elimu vilivyowekwa na VETA, Eng. Luteganya aliongeza kwamba “ wale wote watakaojiunga na VSOMO watatakiwa kufanya mtihani ili kufudhu mafunzo ya vitendo yatakayotolewa na VETA katika vituo vyao nchi nzima. Vyeti vya kuhitimu mafunzo vitatolewa kwa wale watakaofaulu mafunzo katika hatua zote mbili ya nadharia na vitendo. Alithibithisha.

Mkurugenzi
Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (wa pili kushoto) na Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu ya Ufundi (VETA), Geoffrey Sabuni
wakifanya ishara ya uzinduzi wa mafunzo ya stadi za ufundi kupitia
mtandao wa simu ya mkononi yajulikanayo kama “VSOMO” yaani VETA SOMO,
katika hafla iliyofanyika kwenye Chuo cha Veta cha Kipawa jijini Dar es
Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa DTBi, Mhandisi George
Mulamula na (kulia) ni Mkurugenzi wa VETA, Kanda ya Dar es Salaam, Habib
Bukko.

Mkurugenzi
Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (wa pili kushoto) na Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu ya Ufundi (VETA), Geoffrey Sabuni
wakifanya ishara ya uzinduzi wa mafunzo ya stadi za ufundi kupitia
mtandao wa simu ya mkononi yajulikanayo kama “VSOMO” yaani VETA SOMO,
katika hafla iliyofanyika kwenye Chuo cha Veta cha Kipawa jijini Dar es
Salaam jana.

Mkurugenzi
Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso akizungumza katika uzinduzi
wa mafunzo ya stadi za ufundi kupitia mtandao wa simu ya mkononi
yajulikanayo kama “VSOMO” yaani VETA SOMO, katika hafla iliyofanyika
kwenye Chuo cha Veta cha Kipawa jijini Dar es Salaam jana. Kutoka
(kulia) ni Mkuu wa Chuo cha VETA – Kipawa, Mhandisi Lucius Luteganya,
Mkurugenzi wa VETA, Kanda ya Dar es Salaam, Habib Bukko, Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu ya Ufundi (VETA), Geoffrey Sabuni na
Mkurugenzi Mkuu wa DTBi, Mhandisi George Mulamula.

Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu ya Ufundi (VETA), Geoffrey Sabuni
akizungumza katika uzinduzi wa mafunzo ya stadi za ufundi kupitia
mtandao wa simu ya mkononi yajulikanayo kama “VSOMO” yaani VETA SOMO,
katika hafla iliyofanyika kwenye Chuo cha Veta cha Kipawa jijini Dar es
Salaam jana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...