BEKI wa timu ya Kagera Sugar, Ibrahim Job ameanza kuwa lulu huku timu kadhaa zikionekana kuwania saini ya mchezaji huyo huku tayari ameshamalizana na Kagera Sugar baada ya kumaliza mkataba wake wa msimu mmoja kutokana na kuridhishwa na kiwango alichokionesha msimu uliopita.
Job amesema kuwa kuna timu tano za ligi zinazohitaji huduma yake na ameshaanza nazo mazungumzo na kwa upande wake yupo radhi kuitumikia timu yeyote ilimradi tu aridhishwe na dau watakalompatia na nafasi kubwa anaitoa kwa Kagera na endapo watampa dau zuri basi hatokuwa na haja ya kuondoka ndani ya kikosi hicho msimu ujao.
"Nipo radhi kusajiliwa na timu yeyote itakayonipa dau la kuridhisha japokuwa nafasi kubwa naipa timu yangu na endapo watanipa dau nitakaloona linafaa basi nitaendelea kusalia ndani ya kikosi hicho", amesema Job. Ila kikubwa ninachokiangalia ni kupata nafasi ya kucheza na si fedha kwani kipaji chake ni muhimu zaidi kwani siwezi kuangalia fedha alafu nikasugua benchi kwani ninachokitaka ni kupata nafasi itakayoniwezesha watu kuona kipaji na uwezo wangu wa kusakata soka.
Beki huyo ameweza kuisaidia timu yake katika hatari ya kushuka daraja baada ya kupata alama 31 katika msimamo wa ligi huku wakishinda mchezo wao wa mwisho dhidi ya Mwadui kwa goli 2-0.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...