Wapendwa Watanzania wapenzi wa Soka timu yetu FC KILIMANJARO imefululiza kwa ushindi kwa mechi 7 imetoka sare mechi 1 na imefungwa mechi 1.
Ushindi huo umepatikana kwa Ubora na umahiri wa wachezaji wa timu hiyo Pamoja na Baraka zote toka kwa Watanzania wanaoishi nchini Sweden chini
Uongozi wa Mheshimiwa Balozi Dora Msechu ambaye ni Balozi wa Tanzania nchi za Notrdic na Baltic ambaye pamoja majukumu hayo mazito ya kuiwakilisha nchi
pia ni Mama Mlezi wa FC KILIMANJARO.
FC KILIMANJARO wanatuma salaam kwa Mheshimiwa Nape atambue kwamba ana vijana wanaopeperusha Bendera ya Tanzania nchini Sweden pia Salamu nyingine ziwaendee wapenzi wote wa soka nyumbani Tanzania na kwingine Duniani.
Tunaomba support zenu za hali na mali ili timu yetu iweze kufika mbali zaidi.
Salam kabla ya kuanza kwa moja ya mitanange ya FC KILIMANJARO.
Beki akiwa tayari tayari kumdhibiti mpinzani wake.
Kamati ya Ufundi ya FC KILIMANJARO.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...