Serikali imeanza hatua za awali za kufanyia utafiti wa ubora wa picha zinazopigwa na ndege isiyo na rubani katika matumizi ya kuandaa ramani.
Hadi sasa picha zilizopigwa zinaonyesha kuwa nzuri ambapo mafunzo zaidi juu ya matumizi ya picha hizo na jinsi ya kuandaa ramani yanahitajika.
Serikali ya Tanzania na ile ya Korea Kusini zinaendelea na mazungumzo ili Korea iweze kutoa mafunzo na ushauri wa kitaalam kuhusu matumizi ya drones katika kuchora ramani na kuhuisha ramani za siku nyingi.
Kwa kuanzia utaangaliwa uwezekano wa picha hizo kutumiwa kupanga ukuaji wa miji midogo kama Kibaigwa, Uvinza, Chanika na mingineyo ili ikue kimpangilio.
Picha za Angani zilizopigwa na Ndege Isiyo na Rubani (Drone) ambazo zinaaminika kuwa ni bora zaidi ya zile za awali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...