Wawakilishi toka Serikali za mitaa, Serikali ya mkoa na Serikali kuu, sekta binafsi na taasisi za kijamii za kiraia zinakutana leo tarehe 20 Juni mjini Arusha ikiwa ni mkutano wa tatu wa wadau wa mpango mji wa Arusha 2035.

Timu yenye wataalamu kutoka jiji la Arusha,Mkuu wa wilaya wa Arusha na Meru Arusha, tume ya undeshaji ya Mkoa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi watazindua Rasimu ya Mwisho ya Mpango Mji Kabambe wa Arusha 2035 , wakisaidiwa na mshauri mtaalam aliyeteuliwa toka Singapore, Surbana International Consultants Maeneo ndani ya mpango mji itachukua kilometa za mraba 278 za mji wa Arusha na kilometa za mraba 330 zilizochaguliwa za wilaya ya Arusha na Arumeru zikifanya jumla ya kilometa za mraba 608.

Rasimu hii ya Mwisho ya mchoro pendekezi itaonyesha matumizi ya siku zijazo ya ardhi ndani ya eneo linalopangwa . Pamoja na haya utaonyesha mpango mzima wa usafirishaji na barabara, mpango wa aina mbali mbali za barabara, miundombinu na usafirishaji wa mizigo utaelezwa kwa kina.

Hali kadhalika mchoro pendekezi unaoonyesha mpango mzima wa miundombinu utaelezewa kwa kina, hii ni pamoja na mpango kazi na mtandao wa maji safi na maji taka, maji ya mvua, taka ngumu, mfumo wa umeme na mtandao wa mawasiliano ya teknolojia. Maendeleo ya uchumi wa pamoja na ulinzi wa mazingira itakuwa ni sehemu kubwa ya mada. Michoro ya usanifu wa kina utawasilishwa kuonyesha uwezo wa kijamii na kiuchumi wa siku zijazo “Mji Mkuu Kijani wa Afrika Mashariki”.

Uwasilishwaji wa Rasimu na wataalamu utakamilishwa na maelezo ya kina ya “Mpango wa Utekelezaji”. Mpango pendekezi unalenga kuwa wa maono lakini pia uoneshe uhalisia kwa hivyo umuhimu wa uundaji wa hati maalum yakusaidia utelekelezaji wa mpango huu. 

“Rasimu ya mwisho ya michoro ni hatua muhimu kwa mkoa wetu. Mahitaji ya baadaye kwa ajili ya mji wetu unaokua, unatuhitaji kuwa na mipango ya nyumba zaidi, miundombinu bora, mipango ya maendeleo bora kwa ajili ya viwanda, makazi na maeneo ya kijani kwa njia inayojali mazingira. Hii rasimu ya mwisho inatupa fursa ya kuweza kutengeneza mji wa kijani, kitovu cha kanda, na kuonyesha mfano wa ufanisi katika upangaji wa mji” alisema Juma Idd Mkurugenzi wa Jiji la Arusha. 

Mkutano wa kwanza wa wadau ulifanyika Mei mwaka 2015, ulizungumzia mchanganuo wa muktadha wa kanda kwa wadau na pia kupendekeza mtazamo na mpangilio wa siku zijazo wa mamlaka ya jiji la Arusha. Mtazamo wa jumla wa matokeo ya waatalaam ya mkutano wa wadau uliopita utajadiliwa mbele ya wadau watakaokuwepo.

Huu ilifuatiwa na mkutano wa pili wa wadau Novemba 2015, na mkutano wa wataalam Dar es Salaam , Disemba 2015.

Lengo la mkutano huu wa mwisho wa wadau kama ilivyoagizwa na Sheria ya Mipango ya mwaka 2007 ni kuidhinisha hii Rasimu ya mwisho. Hatimaye Rasimu ya Mwisho ya Michoro itatumwa kwa madiwani, kwa Katibu Tawala wa Mkoa na kwa Mkurugenzi wa Mipango Miji kwenye Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Baada ya kuipitia, jamii itapata fursa ya kushiriki kikamilifu, kukusanya maoni na mapendekezo, kabla ya idhini ya mwisho kutoka kwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Hatua hii shirikishi inalenga kupokea mchango muhimu wa kuboresha mpango mji wa Arusha kutoka kwa wadau wote.Wananchi wote watajulishwa mara kwa mara kuhusu hatua za maendeleo za mpango mji kupitia vyombo mbalimbali vya habari ikiwa ni machapisho, na mitandao ya kijamii. Watu wote wanakaribishwa kutoa maoni yao juu ya mpango mji. 

Kupitia Facebook: Arusha 2035, Instagram: Arusha2035 na Twitter: Arusha_2035, kwa kutoa maoni yao kwenye sanduku la maoni katika wilaya na ofisi za kata au baruapepe: arusha2035@gmail.com.

KUHUSU SURBANA
Surbana Consultans Pte. Ltd. Ni kampuni iliyosajiliwa Singapore mwaka 2003 kama kampuni inayofanya biashara ya ushauri wa kitaalam ikitoa huduma kamili za ujenzi, ikiwemo usanifu wa majengo, uhandisi, ukadiriaji majenzi, na usimamizi wa miradi ya ujenzi, coastal engineering and miundombinu, mipango miji, tekinologia ya ujenzi na usimamizi wa miji mikubwa.

Kuanzia hapo, Surbana imefanikiwa kutanua huduma zake za kibiashara katika nchi 30 wakati ikibakia kuongoza katika soko la ujenzi wa nyumba za makazi Singapore. Kwa mchango wake mkubwa katika mazingira yaliyojengwa, Surbana imepokea tuzo mbalimbali ikwepo World Habitat Award na tuzo ya FIABCI Prix D’excellence . Surbana imepewa hadhi ya kuwa moja ya kampuni kumi bora za usanifu wa majengo na ujenzi Singapore na Building and Construction Interchange Asia (BCI Asia).

Kampuni ina uzoefu mkubwa barani Afrika, kuanzia 2005. Miradi yao ni pamoja na mradi uliowapatia tuzo ya mpangomji na kiwango cha kanda cha mipango mji, mji wa Kigali, Rwanda. Surbana kwa sasa inatoa ushauri kwa Serikali ya Tanzania , pia kwa Mpango Mji Kabambe wa Mwanza.

Kwa kuongezea, mipango miji ya Cazenga/Sambizanga nchini Angola, Oyo-Oliombo nchini DRC na Royal Bafokeng, Afrika Kusini.Biashara zote za ushauri na maendeleo ya miji sasa inaajiri zaidi ya watu 2,200 katika miji 17 katika bara la Asia, na mashariki ya kati. Surbana inamilikiwa wa Temasek Holdings (60%) na CapitLand (40%).

Kwa Maelezo Zaidi au Maswali:
Mkurugenzi wa Jiji

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 20, 2016

    The mdudu, hahaaaa yetu macho #Makeke kibao mwisho wa siku #RiP kama ule mji wa#Kigamboni wenye kufanya yao wapo South Africa watu kimya kimya huku watu wakishangaa miji town inavyo mea kama uyoga ila nyie ndugu zangu kwa kujenga kwa mdomo duniani mnashika number 1

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 20, 2016

    Ni mpango mzuri sana ila viongozi wa mkoa mnatakiwa kumaliza matatizo yaliyopo kwanza kabla ya kurukia huu mpango!Hebu angalia migogoro iliyopo NJIRO KITALU E NA F ni AIBU KUBWA KWA JIJI na HASWA HASWA VIONGOZI WAKUU.MKUU WA MKOA NA WILAYA YA ARUSHA MJINI NINYI NI WAGENI HAPA MKOANI HIVYO YAWBIDI KUCHUKUA TAHADHARI MSIJE PONZWA NA VIONGOZI WA JIJI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...