MICHEZO ya tano ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania
(INTERPORTS GAMES) yamemalizika kwa timu ya Bandari ya Tanga kuibuka
Mabingwa wa jumla.
Timu ya Bandari ya Tanga imeibuka kwa kunyakua vikombe 7 ikifuatiwa na Bandari Makao Makuu Dar es Salaam kwa kujinyakualia vikombe 7 ambapo Bandari Mtwara na Bandari za Maziwa kila mmoja kujinyakulia kikombe kimoja kimoja. Akikabidhi vikombe na zawadi mbalimbali kwa washindi Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania, Mussa Msabimana ,aliwapongeza washiriki hao kwa kuonyesha umahiri katika michezo mbalimbali.
Alisema mbali ya umri wao kwenda juu lakini walikuwa wakionekana kama vijana ambao wanaweza kucheza timu yoyote inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara. “Nimefarijika kuwaoma wafanyakazi wenzangu umri tofauti mukicheza mpira na kushindwa kutofautisha kijana na mzee, munakimbia uwanjani kama Messi na Ronaldo” alisema Msabimana .
Aliwataka wanamichezo hao ambao ni watumishi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania kuwa wamoja na kuwa na mshikamano ili kuweza kuyafikia malengo waliojiwekea.
Mshindi wa bao kutoka Bandari Makao Makuu Dar es Salaam, Mwinyi Sultan, akikabidhiwa kombe na Kaimu Mkurugenzi wa Mmlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania, Mussa Msabimana baada ya kuibuka msindi wa mchezo huo wakati wa michezo iliyofanyika Tanga kwa siku 4 viwanja mbalimbali Mkoani humo. Tangakumekuchablog
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...