Katika
kuelekea mwisho wa mwaka 2016 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2017,
Kampuni ya EY Tanzania, imewakutanisha pamoja wafanyakazi wake katika
hafla ya kufunga mwaka iliyofanyika mwishoni mwa wiki, Katika hoteli ya
Hyatt Regency, Jijini Dar es salaam.
Hafla
hiyo, iliyoambatana na zoezi la utoaji wa tuzo kwa wafanyakazi bora wa
mwaka 2016, ilinogeshwa pia na burudani ya muziki kutoka Bendi ya
Malaika chini ya Mwanamuziki Christian Bella anaetamba na nyimbo zake
kadhaa.
Mkurugenzi
Mkazi wa Kampuni ya EY Tanzania, Joseph Sheffu akizungumza katika hafya
hiyo, ambapo aliwapongeza wafanyakazi wake hao kwa namna wanavyofanya
kazi kwa bidii na kujituma, na kuwataka kuongeza bidii zaidi kwa mwaka
ujao.
Baadhi
ya Wafanyakazi wa Kampuni ya EY Tanzania, wakijiandaa kufungua shampein
katika katika hafla ya kufunga mwaka iliyofanyika mwishoni mwa wiki,
Katika hoteli ya Hyatt Regency, Jijini Dar es salaam.
Baadhi
ya Wafanyakazi wa Kampuni ya EY Tanzania, wakigonganisha glass ikiwa ni
ishara ya kutakiana heri ya kufunga mwaka wa kazi katika hafla ya
kufunga mwaka iliyofanyika mwishoni mwa wiki, Katika hoteli ya Hyatt
Regency, Jijini Dar es salaam.

Mwanamuziki
Christian Bella na Bendi yake ya Malaika wakitoa burudani kwa Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya
EY Tanzania, katika hafla ya kufunga mwaka iliyofanyika mwishoni mwa
wiki, Katika hoteli ya Hyatt Regency, Jijini Dar es salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...