
Kampuni ya Paraa Mwanga ambayo siku kadhaa zilizopita ilizindua kampeni ya Tunaangaza Afrika ambayo iliambatana na shindano ambalo litafanyika kwa miezi mitatu ambapo watu mbalimbali watakuwa wakishiriki na kushinda vitu mbalimbali ikiwepo tv, paneli ya sola, redio na king’amuzi cha Continental.
Droo ya kwanza ya kutafuta washindi imefanyika na washindi 11 kupatikana ambapo mmoja wao ameshinda tv ya nchi 24, jiko la gesi, bima ya afya ya mwaka, chaja ya simu, king’amuzi, redio na paneli ya sola na wengine wakishinda redio, flash, paneli ya sola, taa na chaja ya simu.

Washindi waliopatikana katika drroo hiyo ni Lawrance Andrew, Thomas Kimanzi, Abdul Kareem, Clement Mandandi, Ramzan Niga, Issayo Matari, Majaliwa Bondala, Mohammed Issa, Juma Kitenesi na Bernard Mwalangala.
Akizungumza na MO BLOG baada ya kuwatangaza washindi wa droo ya kwanza, Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya Paraa Mwanga, Mwanatumu Mohammed alisema hiyo ni sehemu ya kwanza ya kutafuta washindi wa zawadi ambazo zimeandaliwa kwa ajili ya shindano hilo na kuwataka Watanzania kushiriki kwa wingi ili waweze kushinda zawadi hizo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...