Na Luteni Selemani Semunyu, JWTZ.
Wachezaji wa Golf wa klabu ya Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania ya Lugalo wametakiwa kutobweteka na mfululizo wa ushindi waliopata katika mashindano mbalimbali badala yake wemewatakiwa kujiweka tayari na mashindano ya Kimataifa.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa klabu hiyo Brigedia Jenerali Michael Luwongo mara baada ya kurejea kwa Timu hiyo iliyokuwa ikishiriki Mashindano ya Chairman Troph yaliyofanyika kwa siku Mbili Moshi Mkoani Kilimanjaro ambako ilinyakua vikombe Vinne.
“Najua sie ni Klabu bora ya Golf nchini na yenye wachezaji wazuri kitaifa lakini sasa ni wakati wa kujiandaa Kimataifa ambako tutaitangaza nchi vyema katika mchezo huo na kuliletea Sifa jeshi letu.” Alisema Brigedia Jenerali Luwongo.
Aliongeza kuwa licha ya kuweka maandalizi ya ushiriki wa kimataifa kwa mwaka 2017 lakini ni fursa kwa wanaotaka kujifunza golf wakati huu wa likizo za mwisho wa mwaka kujitokeza klwani shughuli zote za golf katika uwanja wa Lugalo zitaendelea kama kawaida.
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...