Usiku wa manane katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa J.K.Nyerere jijini Dar es salaam jana usiku jicho la kamera ya paparazi lilimzoa mwanamuziki Ebrahim Makunja aka Kamanda Ras Makunja ambaye alikuwa ndio kwanza katua kutokea nchini Ujerumani,mwanamuziki huyo wa kimataifa anayeiongoza bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa Band aka FFU Ughaibuni,alipokumbana na paparazi akutaka maneno zaidi bali alipakiwa katika gari moja jeusi aina na Noa na kutokomea aliko tokomea,ubuyu umedokeza kuwa bendi hiyo ipo likizo kwa muda wa miezi miwili ,likizo hiyo imetokana na kufanya tour miaka miwili bila mapumziko, Kiongozi huyo wa Ngoma Africa band inawezekena yupo nyumbani Tanzania labda kwa likizo kama inavyodhaniwa,Any way Kikamanda Ketu Ras Makunja karibu nyumbani,

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...