Baadhi
ya wakazi wa vijiji vinavyozunguka na mgodi wa almasi katika wilaya ya
kishapu mkoani shinyanga, wameelezea kutoridhishwa na uwepo wa
wawekezaji wa madini katika wilaya hiyo kutokana na mchango wao mdogo
kwenye shughuli za kimaendeleo.
Wakizungumza
na Lake Fm, wakazi hao wamesema bado vijiji vingi wilayani kishapu
vinakumbwa na changamoto kadhaa ikiwemo ukosefu wa huduma za afya, maji,
miundombinu ya umeme pamoja na barabara, na kwamba wajibu wao
kimaendeleo umekuwa mdogo ikilinganishwa na neema ya madini iliyopo
katika wilaya hiyo.
Akizungumzia
wajibu wa wawekezaji hususani wa madini katika maeneo mbalimbali
nchini, Mwanasheria kutoka Taasisi ya Demokrasia na Utawala Bora ADLG,
Carolina Tizeba, amesema sheria ya madini ya Mwaka 2010, kifungu cha 10
inawataka wawekezaji kuwajibika kwa ajili ya maendeleo ya jamii kwenye
maeneo waliyowekeza.
USIKOSE
KUFUATILIA MAKALA YA "MAISHA YA WATU NA RASILIMALI WALIZOPEWA NA
MWENYEZI MUNGU" HIVI KARIBUNI, KUPITIA 102.5 LAKE FM MWANZA NA BMG
HABARI.

Baadhi ya akina mama wa Kijiji cha Ikonongo wilayani Kishapu, wakitoka Kliniki, ambapo baiskeli ni chombo kikuu cha usafiri katika wilaya hiyo.
#BMGHabari
Upendo Hotel ni moja ya hoteli kubwa zilizoko katika Kijiji cha Nyenze wilayani Kishapu.
Baadhi ya wakazi wa wilaya ya Kihapu wakimuaga mwandishi wa habari hii (hayupo pichani).


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...