Kituo cha kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi cha Amani, chenye makao makuu yake mkoani Kilimanjaro kimetunukiwa tuzo ya Uongozi bora kwa mashirika yasiyo ya kiserikali Afrika, mwaka 2016. Sherehe ya kutunukiwa tuzo hii ilikuwa ni sehemu ya mkutano wa siku mbili uliofanyika katika hoteli ya Le Meridian huko Mauritius kuhusiana na Uongozi Afrika. 

Amani imepokea tuzo hii kutokana na mbinu bora inazozitumia kuwawezesha mamia ya watoto wanaoishi kwenye mazingira hatarishi kupata haki zao za msingi kielimu na maisha bora kwenye familia na jamii zao kwa baadae. Tuzo hii imepokelewa tarehe 7.12.2016 kwa niaba ya uongozi wa Amani na Dr. Juliette Biao Koudenoukpo, (Mkurugenzi wa kanda ya Afrika – Umoja wa Mataifa, UNEP. Mkutano huu wa Uongozi wa Afrika na Tuzo hizi ni jitihada za kundi kubwa la wafanyabiashara wa kimataifa walioko chini ya siku ya kuadhimisha mahusiano ya makampuni ya kibiashara na jamii (World CSR Day) na wanaofanya vizuri katika tathnia hii.

Zaidi ya viongozi mia moja wa wafanya biashara wa kimataifa, watendaji wakuu, maraisi na makamu wakuu wa vyuo vikuu mbalimbali Afrika na viongozi waandamizi wa serikali wamehudhuria mkutano huu.
Dr. R. L. Bhatia, Muanzilishi wa siku ya mahusiano ya makampuni ya kibiashara na jamii duniani na Mwenyekiti wa Jopo alisema: “Uongozi wa Amani ni imara na umeonyesha uongozi bora uliotukuka katika kufikia malengo ya shirika na kubadilisha maisha ya watoto walitoka kwenye mazingira hatarishi nchini Tanzania. 

Amani ina sifa ya kipekee na mikakati imara ya kuendelea kuwasaidia watoto hawa siku za usoni. Sisi kama jumuiya ya wafanyabiashara wa kimataifa tunajivunia kutoa tuzo hii kwa kituo cha Amani na tunafurahi kusherehekea mafanikio yao.”

Meindert Schaap, Mkurugenzi Mtendaji wa Amani alisema: “Kwasasa tunafanya kazi na watoto waliotoka kwenye mazingira hatarishi 345, wakiwemo watoto wa kike na wakiume, na tunafanya kazi kwenye miji mitatu Tanzania ambayo ni Moshi, Arusha na Singida. Zaidi ya watoto 250 waliotoka kwenye mazingira hatarishi wanasaidiwa kupata elimu na kituo cha Amani. 
Tuzo hii imetupa utambulisho mkubwa kwa jamii kwa kutambua umuhimu wa kazi zetu kwenye jamii na imetutia moyo wa kuendelea kutanua wigo wetu ili kuweza kuwafikiwa watoto wengi zaidi wanaoishi kwenye mazingira hatarishi hapa nchini.”

“Kwa kuchaguliwa kupata tuzo hii na kundi la viongozi wa wafanyabishara wa kimataifa duniani inatudhihirishia kuwa Amani tunafanya shughuli zetu kwa weledi mkubwa. Hii inathibitisha ni jinsi gani Amani inafanya kazi yake katika hali nyoofu, uaminifu na uweledi kwa kiwango cha juu kuwasaidia mamia ya watoto kutoka kwenye mazingira hatarishi kwa mafanikio.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...