Na Evelyn Mkokoi - Bagamoyo
SERIKALI imeiagiza Baraza la hifadhi ya Mazingira (NEMC ) na Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais kufanya tathimini
ya awali ya kuangalia ni namna gani itaweza kuzuia maji ya bahari kuingia katika Taasisi ya Sanaa na
Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) na kuharibu miundombinu yake ambapo hadi sasa takribani mita
70 hadi 100 ya bahari imeisogelea taasisi hiyo.
Akizungumza jana wilayani Bagamoyo,Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na
Mazingira Luhaga Mpina wakati wa ziara ya kutembelea Taasisi hiyo na kujionea ni namna gani
bahari inavyosogea katika taasisi hiyo na kuanza kuathiri baadhi ya majengo.
Alisema kutokana na hali hiyo kuwa ya dharura ameziagiza mamlaka hizo kufanya tathimini ya awali
ambapo kufikia Januari 30 mwakani watapaswa kukabidhi ripoti ya awali kwa serikali na kujua nini
kifanyike katika kunusuru taasisi hiyo na kuifanya mahala pazuri pa kujifunzia masuala ya utamaduni.
Mpina alisema ripoti hiyo itaweza kupelekwa serikalini ili mipango madhubuti ianze kufanyika ya
kuhakikisha taasisi hiyo inakuwepo na inaendelea kutoa mafunzo yake kama kawaida bila kuathiriwa
na usogelewaji wa bahari katika maeneo hayo.
Naibu Waziri
Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina Pamoja na
ujumbe wake na Viongozi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo wakiangalia
eneo la fukwe la chuo icho ilivyoliwa na bahari ikiwa ni athari zitokanazo na
mabadiliko ya tabia nchi.Dkt Herbert Makoye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni ya Bagamoyo akiongea na vyombo vya habari kuhusu uhabifu wa fukwe utokanao na athari za mabadiliko ya abia nchi.
Naibu Waziri
Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina Kiongea na
Vyombo vya Habari katika fukwe ya Bagamoyo upande wa Taasisi ya Sanaa,namna
ambayo majengo matatu ya chuo hicho yapo hatarini kumezwa na bahari kutokana na
athari za mabadiliko a tabia nchi na kuomba msaada wa kitaalam kwa serikali
hususan Ofii ya Makamu wa Rais. (Picha na Evelyn Mkokoi OMR).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...