Watoto 108 wanaoisha katika mazingira magumu wanaolelewa katika kituo cha”Watoto Wetu Tanzania”(WWT),kilichopo Kimara Suka jijini Dar es Salaam,pamoja na walezi wao wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa benki ya CBA walipotembelea kituo hicho kutoa msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo vyakula na nguo.
Mwanzilishi na Mkuu wa Kituo cha kulelea watoto wanaishi katika mazingira magumu wa kituo cha”Watoto Wetu Tanzania”(WWT) kilichopo Kimara Suka jijini Dar es Salaam, Evance Tegete akikabidhiwa msaada wa mfuko wa sabuni na Meneja Masoko wa Benki ya CBA,Salomon Kawiche(kulia) wakati wafanyakazi hao walipotembelea kituo hicho kutoa msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo vyakula na nguo.
Meneja Uhusiano wa Banki ya CBA, Anna Shirima (kulia) akisaidiana na watoto wanaolelewa katika kituo cha”watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha “Watoto Wetu Tanzania”(WWT) kilichopo Kimara Suka jijini Dar es Salaam,kuweka vyakula pamoja, baada ya kukabidhiwa na wafanyakazi wa benki hiyo msaada huo wa vitu mbalimbali vikiwemo vyakula na nguo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...