Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria Bw. Aloyce Mwogofi (aliyesimama kushoto) akiongea katika Kikao na watumishi wa Wizara hiyo wakati wakipokea taarifa ya mapendekezo ya sheria ya Ndoa ya 1971 na utungwaji wa sheria ya msaada wa kisheria, leo katika ukumbi wa wizara hiyo.
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria wakimsikiliza kwa makini mtoa taarifa ya mapendekezo ya sheria ya Ndoa ya 1971 na utungwaji wa sheria ya msaada wa kisheria Bw Sabath Cazmiry (wa tatu kushoto), leo katika ukumbi wa wizara hiyo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria Bw. Amon Mpanju (kushoto) akisisitiza jambo kwa watumishi wa Wizara hiyo wakati wa kikao cha kupokea taarifa ya mapendekezo ya sheria ya Ndoa ya 1971 na utungwaji wa sheria ya msaada wa kisheria leo, katika ukumbi wa wizara hiyo.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...