Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia huduma yake inayokuwa
kwa kasi ya Airtel Money imezindua na kuitambulisha kampeni kabambe
ya Mr Money ijulikanayo kama Relax.. Airtel Money ndio mambo yote.
Akiongea
kuhusu Kampeni hiyo Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema
“Kupitia huduma ya Airtel Money wateja wetu wanafaidika na mambo lukuki ikiwemo
“Kupitia huduma ya Airtel Money wateja wetu wanafaidika na mambo lukuki ikiwemo
Kutuma pesa kwenda mitandoa yote kwa bei nafuu
wateja
wetu wanaweza kutuma pesa kwenda mitandao mingine kwa tozo ileile
wakati wowote mahali popote pale nchini. Haya ni mapinduzi ya kipekee
katika huduma za kifedha ambapo tumewezesha
wateja wetu kufanya miamala hiyo kwa urahisi zaidi bila kujali gharama.
Kupata vifurushi bora kupitia Airtel Money OFA KABAMBE vyenye ujazo zaidi kuliko vifurushi vya mitandao mingingine yote:
Kupata hii piga *150*60# kisha nunua kifurushi kupia Airtel Money kwa kuchagua
No.6 OFA KABAMBE , Pia vipo vifurushi vya UNI packs sasa
vinapatikana kupitia huduma ya Airtel Money hivyo kuwawezesha wanafunzi
kujiunga na vifurushi hivyo kwa urahisi zaidi
Kutuma pesa kwenda benki na kutoa pesa kutoka kwenye akaunti yako ya Airtel Money kwenda Benki-
sasa wateja wa Airtel Money wanaweza kufanya miamala hiyo kwenye benki 38 ambazo tayari tunaushirikiano nazo.
Kadhalika wateja waweza kutumia ATM za umoja switch na CRBD zaidi ya
1105 nchini kwa kutoa pesa kwenye akaunti zao za Airtel Money masaa 24
kila siku.
ushirikiano huu umeongeza idadi ya mawakala na kurahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha kupitia simu za mkononi.
Na pia tunawewezesha wateja wetu kupata mikopo ya Timiza isiyo na dhamana kwa
wateja wetu
na mawakala nchini, Mteja anaweza kuomba mkopo wa hadi laki 5 na
kujipangia yeye mweye alipe lini SIKU, WIKI au baada ya MWEZI. Airtel
Timiza ni suluhisho kwa mahitaji ya mikopo ya haraka ya kutatua
changamoto za kijamii lakini pia inawawezesha wajasiriamali
wadogo wadogo kupata mitaji kwaajili ya biashara zao papo hapo.
“Ndio maana tunaseme?
Relax Airtel Money mambo yote” alisisitiza Mmbando
Huduma
ya Airtel Money, kwa sasa imefanikiwa kwa kufanya mihamala mingi ya
kifedha nchini hasa katika maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma za
kibenki. Mwezi uliopita Airtel
Money pia ilifanikiwa kugawa gawio la shilingi bilioni 3.5 kwa
watejawake wote wanaotumia huduma ya Airtel Money.
Meneja Uhusiano wa Airtel akitambulisha kampeni kabambe ya Mr Money ijulikanayo kama Relax.. Airtel Money ndio mambo yote. Kupitia huduma ya Airtel Money wateja wetu wanafaidika na huduma nyingi zenye faida zaidi kwa kupiga tu *150*60#



Kwa mara ya kwanza baada ya mda mrefu wa kufanya makosa Airtel mmeweza sasa kuanzisha kampeni ktk mida muafaka. hongereni
ReplyDelete