Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia huduma yake inayokuwa kwa kasi ya Airtel Money imezindua na  kuitambulisha kampeni  kabambe  ya Mr Money ijulikanayo kama Relax.. Airtel Money ndio mambo yote.
Akiongea kuhusu Kampeni hiyo Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema
“Kupitia huduma ya Airtel Money wateja wetu wanafaidika na mambo lukuki ikiwemo
Kutuma pesa kwenda mitandoa yote kwa bei nafuu wateja wetu wanaweza kutuma pesa kwenda mitandao mingine kwa tozo ileile wakati wowote mahali popote pale nchini. Haya ni mapinduzi ya kipekee katika huduma za kifedha ambapo tumewezesha wateja wetu kufanya miamala hiyo kwa urahisi zaidi bila kujali gharama.
Kupata vifurushi  bora kupitia Airtel Money OFA KABAMBE vyenye ujazo zaidi kuliko vifurushi vya mitandao mingingine yote: Kupata hii piga *150*60# kisha nunua kifurushi kupia Airtel Money kwa kuchagua No.6 OFA KABAMBE  , Pia vipo vifurushi vya UNI packs sasa vinapatikana kupitia huduma ya Airtel Money hivyo kuwawezesha wanafunzi kujiunga na vifurushi hivyo kwa urahisi zaidi

Kutuma pesa kwenda benki na kutoa pesa kutoka kwenye akaunti yako ya Airtel Money kwenda Benki-  sasa wateja wa Airtel Money wanaweza kufanya miamala hiyo kwenye benki 38 ambazo tayari tunaushirikiano nazo. Kadhalika wateja waweza kutumia ATM za umoja switch na CRBD zaidi ya 1105 nchini kwa kutoa pesa kwenye akaunti zao za Airtel Money masaa 24 kila siku. ushirikiano huu umeongeza idadi ya mawakala na kurahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha kupitia simu za mkononi.
Na pia tunawewezesha wateja wetu kupata mikopo ya Timiza isiyo na dhamana  kwa wateja wetu na mawakala nchini, Mteja anaweza kuomba mkopo wa hadi laki 5 na kujipangia yeye mweye alipe lini SIKU, WIKI au baada ya  MWEZI. Airtel Timiza ni suluhisho kwa mahitaji ya mikopo ya haraka ya kutatua changamoto za kijamii lakini pia inawawezesha wajasiriamali wadogo wadogo kupata mitaji kwaajili ya biashara  zao papo hapo.
“Ndio maana tunaseme? Relax Airtel Money mambo yote” alisisitiza Mmbando

Huduma ya Airtel Money, kwa sasa imefanikiwa kwa kufanya mihamala mingi ya kifedha nchini hasa  katika maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma za kibenki. Mwezi uliopita Airtel Money pia ilifanikiwa kugawa gawio la shilingi bilioni 3.5 kwa watejawake wote wanaotumia huduma ya Airtel Money.


Meneja Uhusiano wa Airtel akitambulisha kampeni  kabambe  ya Mr Money ijulikanayo kama Relax.. Airtel Money ndio mambo yote. Kupitia huduma ya Airtel Money wateja wetu wanafaidika na huduma nyingi zenye faida zaidi kwa kupiga tu *150*60#

  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kwa mara ya kwanza baada ya mda mrefu wa kufanya makosa Airtel mmeweza sasa kuanzisha kampeni ktk mida muafaka. hongereni

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...