Mkurugenzi wa Friedkin Conservation Fund (FCF), Abdulkadir Mohamed (wa tatu kulia) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka (wa pili kulia) shehena ya mifuko 3000 ya saruji ikiwa ni jitihada za kampuni hiyo kusaidia ujenzi wa shule za sekondari wilayani Meatu. Kampuni hizo Mwiba Holdings na Tanzania Game Trackers pia zimekubali kusaidia mabati 1000 ikiwa ni msaada. Wengine ni viongozi mbalimbali walioshiriki katika tukio hilo Mkurugenzi wa Friedkin Conservation Fund (FCF), Pratik Patel akizungumza katika tukio la kampuni hiyo kukabidhi shehena ya mifuko 3000 ya saruji ikiwa ni jitihada za kampuni hiyo kusaidia ujenzi wa shule za sekondari wilayani Meatu. Kampuni hizo yaani Mwiba Holdings pamoja na Tanzania Game Trackers pia zimekubali kusaidia mabati 1000 kama msaada Mkurugenzi wa Friedkin Conservation Fund (FCF), Abdulkadir Mohamed (kulia) akimtamkia Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka (kushoto) kuwa mbali na kampuni hiyo kutoa mifuko 3000 ya saruji kusaidia ujenzi wa shule za sekondari wilayani Meatu. Wataongeza msaada wa mabati 1000. Wengine ni Miss Universe Tanzania 2016/17, Jihan Dimack (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa FCF, Pratik Patel (wa pili kulia) wakishuhudia tukio hilo.

 KAMPUNI kitalii zilizo chini ya Friedkin Conservation Fund (FCF) Tanzania iliyowekeza katika pori la Makao wilayani Meatu na Maswa Mkoani Simiyu imechangia mifuko 3000 ya saruji na mabati na 1000 kusaidia ujenzi wa shule za sekondari wilayani humo. Misaada hiyo yenye thamani ya zaidi ya sh milioni 70 imetolewa na kampuni hizo ikiwa ni kuunga mkono mkakati wa serikali ya awamu ya tano ya Rais Dk. John Magufuli kuendeleza elimu ya hasa katika maeneo ya wafugaji ambako kampuni hizo zinafanya shughuli za uwindaji wa kitalii. 

Kampuni zilizokabidhi misaada hiyo juzi katika sherehe zilizofanyika mjini hapa ni pamoja na Mwiba Holdings na Tanzania Game Trackers ambazo kwa pamoja zimetoa saruji hiyo yenye thamani ya sh milioni 48 na mabati yakiwa na thamani ya sh milioni 25. Vifaa hivyo vya ujenzi vitatumika kujenga vyumba vya madarasa na mabweni kwa ajili ya shule zitakazotumiwa na watoto wa jamii za wafugaji zinazoishi jirani na maeneo ya shughuli za uwindaji wa kitalii wilayani Meatu katika mkoa wa Simiyu. Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka (kushoto) akifurahia tamko la Mkurugenzi, Abdulkadir Mohamed (hayupo pichani) kuahidi kuongeza msaada wa mabati 1000 huku Miss Universe Tanzania 2016/17, Jihan Dimack akikabidhiwa kipaza sauti kurudia kauli ya neema za mabati 1000 toka FCF

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...