Na Bashir Yakub.

Wenye nyumba hawako salama ikiwa wapangaji wao ni wahusika wa dawa za kulevya. Ni muhimu kulijua hili ili kujihadhari na kile ambacho kinaweza kukuletea madhara. Sheria mpya ya kupambana na kuzuia dawa za kulevya “The Drug Control and Enforcement Act, No 5 of 2015” imeeleza kwa mapana uhusika wa watu wa kada mbalimbali katika dawa za kulevya.

Tunachotakiwa kujua ni kuwa uhusika haumlengi tu yule mwenyewe mhusika halisi bali umeelekezwa mbali na hata kufika kwa wenye nyumba au wamiliki wa nyumba/eneo.

Pia uhusiano katika sheria hii haumlengi tu mwenye nyumba na mpangaji wake, bali pia mwenye nyumba na wale walio katika nyumba yake wawe watoto, mke, ndugu, rafiki n.k., madhali ni watu wako katika nyumba yako au eneo unalomiliki basi watakuhusu katika hili .

Hata hivyo kabla ya kuona hatia ya mwenye nyumba/eneo tutizame kwanza ni vitu gani vinaitwa dawa za kulevya ili kama unajihadhari ujue lipi la kujihadhari nalo.

1.NI VITU GANI VINAITWA DAWA ZA KULEVYA.

Sheria ya Kupambana na dawa za kulevya inataja aina nyingi mno ya vitu ambavyo imeviita dawa za kulevya. Vipo jamii ya kimiminika, jamii ya unga, jamii ya miti, majani, mbegu n.k.

Kifungu cha 2 cha sheria hiyo kinachosomwa sambamba na Schedule ya 1 ya sheria hiyohiyo kimeorodhesha zaidi ya sampuli 100 ya vitu ambavyo vinahesabika kuwa ni dawa za kulevya hapa Tanzania. Humo imo pia bangi, mirungi, cocaine, heroine, mandrax, morphine, cannabis resin au opium,coca leaf, alphaprodine, etorphine n.k.

Ni vigumu kuzitaja kwa Kiswahili lakini pia ni vigumu kuzitaja zote kwa kuwa ziko zaidi ya mia. Muhimu ni kuwa jihadhari na mienendo ya wapangaji au wale uliowaweka katika nyumba/eneo lako. 

Pia ujue kuwa mirungi nayo ni dawa za kulevya tofauti na wengi wanavyodhani kuwa ni kiburudisho cha starehe halali kama ilivyo sigara au vingine. 

2. HATIA YA MWENYE NYUMBA IKIWA MPANGAJI ANAHUSIKA NA DAWA ZA KULEVYA.

Kifungu cha 19 ( 1 ) cha sheria hiyo kinakataza mmiliki wa muda au wa kudumu kuruhusu eneo lake kutumika kwa namna yoyote katika shughuli yoyote ya dawa za kulevya.

Mmiliki wa muda anaweza kuwa muangalizi wa nyumba labda ameachiwa jukumu hilo na mmiliki halisi au anaweza kuwa mpangaji aliyempangisha mpangaji mwingine( sublease). Wote hawa wanaweza kuwa na hatia katika kifungu hiki.

Mmiliki wa kudumu ndiye mmiliki halisi wa nyumba/eneo. Huyu naye anawajibika katika kifungu hiki. 

KUSOMA ZAIDI sheriayakub.blogspot.com.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...