Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
CHAMA cha Kutetea Abiria (Chakua)
kimewaomba abiria wanaongia katika kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani cha ubungo kutoa sh. 200 kwa ajili ya
kusaidia chama hicho.
Akizungumza na waandishi habari
jijini Dar es Salaam,Mratibu wa chama hicho, Monday Likwepa amesema kuwa chama
kimekuwa na msaada mkubwa kwa abiria hivyo chama kinahitaji kujiendesha na
wadau ni abiria kuchangia kiwango hicho.
Amesema kuwa kiwango hicho walichopanga kitasaidia kuendesha shughuli za
ofisi pamoja na kuweza kushughulika na matatizo ya abiria pale wanapopata
usafiri.
Likwepa amesema kuwa abiria wamekuwa
wakipata matatizo na kukimbilia chakua hivyo kwa utaratibu wa kuchangia
wanawajibu kudai haki zao pale wanapopata usumbufu.
Aidha amesema kuwa wataendelea kutoa
elimu zaidi juu ya uchangiaji wa fedha hiyo katika kituo cha ubungo ili
wananchi wajue uchangiaji huo na pamoja
na faida zake.
Mratibu Mtendaji wa Chama Cha Kutetea Abiria(Chakua), Monday Likwepa
akizungumza na waandishi wa habari juu ya kuchangia abiria wanaosafiri katika kituo kikuu cha mabasi
Ubungo sh.200 kwa ajili kuendesha shughuli za utetezi wa abiria pale anapopatwa
na tatizo. Kushoto ni Mratibu mtendaji wa Chakua, Elias Kalinga na kulia ni Mwenyekit wa wa Taifa wa Chakua, Hassan Mchanjawa.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...