Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha

MKE wa rais mstaafu ,mama Salma Kikwete,amesema mkoa wa Pwani upambane na mafataki wanaoteka fikra za watoto wao wa kike ili kuondokana na mimba za utotoni ambapo mkoa huo ni kati ya mikoa kumi inayoongoza kwa mimba hizo kitaifa.

Aidha amekemea tabia inayofanywa na mashuga dadi wanaojiona mahodari wa kutongoza na kunyemelea watoto wa kike wanafunzi na wengine kuwakatisha masomo kwa kuwatia mimba na kudai anaejiona hodari wa kutongoza dunia aende kwa wanawake wakubwa huko mitaani.

Pamoja na hilo,Mama Salma ,ameitaka jamii kuachana na mila na desturi zinazochochea mimba ,na kusema lazima zitazamwe ili kuwawezesha watoto hao waendelee na masomo yao.

Aliyasema hayo,wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike kimkoa,yaliyofanyika wilayani Kibaha mkoani Pwani,ambayo yamefadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la Room To Read.

MKE wa rais mstaafu ,mama Salma Kikwete ,akiwa katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike kimkoa Mkoani Pwani yaliyofanyika Kibaha na kufadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la Room To Read linalotekeleza mradi wa kumwendeleza mtoto wa kike.Picha na Mwamvua Mwinyi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...