Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) wanatarajia kukaa katika kikao cha kamati ya utendaji ambacho kitaketi Jumamosi Februari 17,mwaka 2018 kwenye Hoteli ya Sea Scape,Mbezi Beach,Dar es Salam.
Ofisa habari wa TFF, Clifford Ndimbo amesema kikao hicho cha kila baada ya miezi mitatu ambacho ni cha kawaida kitakuwa na ajenda kwa mujibu wa Katiba ya TFF kupitia na kutathmini utendaji wa Shirikisho.
Ndimbo amesema kikao hicho cha kamati ya Utendaji kinatanguliwa na vikao vya kamati mbalimbali za TFF ambazo zimeanza kukutana kwa wiki mbili na wiki hii vikao vya kamati hizo kamati ya Sea Scape.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...