Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii.

BAADA ya kesi ya matumizi ya madawa ya kulevya inayomkabili aliyekuwa mlimbwende wa Tanzania 2006 na msaniiwa filamu hapa nchini, Wema Sepetu na wenzake watatu kunguruma kwa takribani mwaka mmoja, leo Machi 12, upande wa mashtaka umefunga ushahidi wao.

Hatua hiyo imekuja baada ya mashahidi watano wa upande wa mashtaka kumaliza kutoa ushahidi wao na kuiachia mahakama katika maamuzi.

Baada ya mahakama kupata taarifa hiyo kutoka kwa Wakili wa serikali, Constantine Kakula, wakili wa Utetezi, Albert Msando aliiomba mahakama kuwasilisha hoja zao za kuishawishi mahakama kuwa washtakiwa wote hawana kesi ya kujibu.


Miss Tanzania 2006 na Msaanii wa filamu, Wema Sepetu akitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo mara baada ya kusomewa mashtaka yanayomkabiri ya Madawa ya kulevya.Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

" Mheshimiwa tunaomba kujenga hoja kwa washtakiwa wote watatu kuwa hawana kesi ya kujibu kuhusiana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapa na upande wa mashtaka, amedai Wakili Msando.
Kifuatia ombi hilo, Hakimu Simba ameutaka upande wa utetezi kuwasilisha hoja zao Machi 23, mwaka huu na kesi hiyo itatajwa tena Aprili 3, mwaka huu.

Kabla ya upande wa mashtaka kuifunga kesi yao waliwaita mashahidi wawili kutoa ushahidi ambao ni,  Steven Ndondo mjumbe wa shina namba 39 eneo la Basihaya na askari D 603 Ditektivu Koplo Robert (31).

Katika ushahidi wake,  Ndondo akiongozwa na Wakili wa Serikali, Costantine Kakula amedai kuwa Februari 4,2017 saa 10 jioni alipigiwa simu na mtu asiyemfahamu kuwa anahitajika mtaa wa Nazareti nyumbani kwa Wema kwa ajili ya kufanya upekuzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...